Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Shehena ya Samaki yanaswa ikisafirishwa
Habari Mchanganyiko

Shehena ya Samaki yanaswa ikisafirishwa

Samaki aina ya Sato wanaopatikana Ziwa Victoria, Mwanza
Spread the love

SHEHENA ya samaki aina ya Sangara tani tatu zenye thamani ya Sh. 19 milioni imekamatwa jijini Mwanza baada ya maofisa wa uvuvi kuanza msako wa watu wanaojihusisha na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, anaandika Moses Mseti.

Msako huo umefanywa baada ya Dk. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo, Mifungo na Uvuvi kuwatupia lawama maofisa wa uvuvi Kanda ya Ziwa kushindwa kudhibiti uvuvi haramu.

Oparesheni hiyo inayoendeshwa katika Ziwa Victoria imekamata sangara waliokaushwa lakini wasiopaswa kuvuliwa chini ya sheria ya 22 ya mwaka 2003 inayozuia Sangara wachanga.

Akizungumza leo mbele ya Dk. Leonard Masale, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Lameck Mongo ambaye ni Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi na Uvuvi Kanda ya Mwanza, amesema samaki hao walikamatwa katika eneo la Nyakalilo, wilayani Sengerema.

Mongo amesema kuwa, samaki hao wenye jumla ya kilo 38,00 sawa na tani tatu, wametaifishwa na kutolewa kwa makundi mbalimbali ikiwemo Gereza la Butimba, kituo cha wazee Bukumbi, shule ya wavulana na wasichana Bwiru na Kituo cha kulelea watoto cha Rescure (TCRC).

Amesema kuwa, samaki waliovuliwa walikuwa na ukubwa wa sentimita 50 ambapo ni wachanga na wasiofaa kuvuliwa.

Ameeleza kushangazwa na hatua ya raia wa kigeni kuingia nchini na kununua kisha kusafirisha samaki wenye ukubwa huo.

“Tumekamata samaki aina ya sangara wachanga na tayari walikuwa wamekaushwa kilo 38,00 ambao bado ni wachanga wasioruhusiwa kuvuliwa,” amesema Mongo.

Mongo amesema kuwa, pamoja na samaki hao kuvuliwa kwa mjibu wa sheria ya 22 ya mwaka 2003, bado unasababisha uchumi wa Taifa kushuka kwa kuwa, watoroshaji hao huwa hawalipi kutokana na kufanya magendo.

Dk. Leonard Masale, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amewaonya raia wa kigeni wanaoingia nchini na kujihusisha na shughuli za ulanguzi wa samaki na kuzisafirisha kwenda nje ya nchi kinyume na taratibu zilizopo.

Dk. Masale amewataka pia viongozi wa vijiji na vitongoji, kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya watu wanaojihusisha na uvuvi haramu na watu wanaosafirisha samaki nje ya nchini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

“Pia samaki hizi tunazogawa hapa, ninawaomba ziwafikie walengwa na tusisikie mgao huu umebadilishwa matumizi na ukaenda sehemu nyingine,” amrsema Dk. Masale.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!