October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shamte afariki dunia

Salum Shamte

Spread the love

SALUM Shamte, Mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Katani Limited, amefariki dunia afajiri ya leo tarehe 30 Machi 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alikokuwa anapatiwa matibabu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa mapema leo na Mariamu Shamte, mke wa marehemu Shamte.

Patrick Mvungi, Msemaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, amesema marehemu Shamte amefariki dunia akiwa anapigania maisha yake, katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).

Mvungi amesema walimpokea Shamte katika taasisi hiyo tarehe 23 Machi 2020, ambapo tarehe 26 Machi mwaka huu, hali yake kiafya ilibadilika na kuhamishiwa ICU hadi umauti ulipomfika.

Kabla ya umauti kumfika, Shamte alikuwa mahabusu akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Sh. 1.14 bilioni kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika (Amcos).

Marehemu Shamte alipandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kuhusu tuhuma hizo, tarehe 31 Oktoba 2019.

Shamte aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi Binafsi Tanzania (TPSF).

error: Content is protected !!