May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Shamsi Nahodha ataka urais Z’bar

Spread the love

SHAMSI Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Mwanasiasa huyo mkongwe, amechukua fomu hiyo leo asubuhi tarehe 18 Juni 2020, katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.

“Nakishukuru chama changu kwa yote kilichonifanyia kwa muda wote, na kunipa heshma hii kubwa ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama chetu cha mapinduzi.

“Nina hakika, watu wengi na wanachama wengi wangetamani sana Mwenyezi Mungu awape fursa hii, wengine watafanikiwa na wengine hawatafanikiwa,” amesema Nahodha muda mfupi baada ya kuchukua fomu.

Nahodha aliyehudumu nafasi ya Waziri Kiongozi katika Serikali ya Zanzibar kwa miaka 10 (2000 – 2010), anakuwa mgombea wa sita akitanguliwa na makada wengine wa chama hicho ambao ni Hussein Ali Mwinyi, Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa na Balozi Ali Karume.

error: Content is protected !!