Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Shambulio la makombora ya Urusi laua 53
Kimataifa

Shambulio la makombora ya Urusi laua 53

Spread the love

RAIA 53 wameuawa katika shambulio la kombora la Urusi katika kijiji kilichopo mashariki mwa Syria Al-Shafah, kundi la uangalizi linasema.

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu Syria lililo na makao yake Uingereza (SOHR) linasema 21 kati ya wanaoripotiwa kuuawa Jumapili ni watoto.

Kijiji hicho kipo Deir al-Zour, mojawapo ya majimbo ya mwisho ambako wangambo wa Islamic State wanendelea kudhibiti ardhi.

Awali SOHR lilisema watu 34 wameuawa katika makombora yaliolenga makaazi ya watu. “Idadi hiyo imeongezeka baada ya kuondolewa kifusi baada ya operesheni ya siku nzima ya uokozi,” Rami Abdel Rahman amesema.

Awali Urusi ilithibitisha kwamba walipuaji wasita wa mabomu ya masafa marefu walitekeleza mashambulio ya angani katika eneo hilo, lakini ikasema iliwalenga wanamgambo na ngome zao.

Urusi ni mshirika wa karibu wa rais wa Syria Bashar al-Assad katika vita vya muda mrefu vya kiraia nchini humo.

Mazungumzo ya amani yanayoungwamkono na Umoja wamataifa yanatarajiwa kuanza upya Geneva wiki ijayo, lakini awamu kadhaa za mazungumzo hayakufuwa dafu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!