Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari Shaka CCM tusipoteze muda  wa malumbano
HabariSiasa

Shaka CCM tusipoteze muda  wa malumbano

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amewataka wana CCM kutopoteza muda kwa malumbano na majibizano kwa kuwa kuna kazi muhimu mbele yao ya kujenga Chama na nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wameanza vizuri uongozi katika kuwatumikia wananchi, hivyo ni jukumu la wana CCM na Watanzania kwa jumla kuwaunga mkono.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amewataka wale wenye tamaa ya kutaka vyeo kujitafakari na kuchapa kazi kwa kuwa kazi kubwa Sasa ni kuijenga nchi.

Shaka aliyasema hayo jana tarehe 10 Disemba, 2022 katika mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Hussein Ali Mwinyi yaliyofanyika katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar (Kisiwandui) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

“Niwaombe wana CCM wenzangu tusipoteze muda wa marumbano, tuna kazi ya kukijenga Chama tuna kazi ya kuijenga nchi, tuna kazi ya kuijenga Zanzibar hii. Dk. Mwinyi ameanza vizuri jasiri mwongoza njia lazima wafuasi tufuate…bega kwa bega,” alisema.

Shaka alisema Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kipo katika mikono salama chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi na kusimamia maendeleo ya wananchi.

“Makamu Mwenyekiti umekabidhiwa jahazi hili hatuna wasiwasi na wewe, umekabidhiwa jahazi hili likiwa salama ‘inshallah’ (Mungu akipenda) utatuvusha…wewe ni nahodha jabari, wewe ni nahodha makini utatuvusha. Wasiojua waanze kupata salamu tunakuja na Dk. Mwinyi,” alisema.

Katibu Mwenezi Shaka alisema moja ya mambo ambayo CCM haijawahi kukosea ni katika kuwapata viongozi makini wa kuivusha nchi.

Shaka alisema kasi ya Rais Dk. Mwinyi imeanza kuwatisha baadhi ya watu waliokuwa na tamaa ya madaraka ambao sasa wameanza kutapatapa.

“Nimesikia kwamba wanafikiria sijui watasusa, msuse msisuse shughuli ipo,” alisema.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais Abdullah ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumza katika mapokezi hayo, alisema serikali itashirikiana na Chama katika kukoleza kasi ya maendeleo.

Abdullah alisema baada ya Dk. Mwinyi kupewa dhamana ya kuongoza Chama upande wa Zanzibar sasa kazi ni moja tu ya kuhakikisha wanasimia mendeleo ndani ya Chama na serikali.

“Niwaombe sana wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, viongozi sote tuliopo hapa tukijenge Chama chetu, tuisimamie serikali yetu tufikie malengo tuliyojiwekea. Majungu, fitina, wanaotaka vyeo havina nafasi,” alisema.

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. …

    MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA…

    MHE. KULE ULIKOOA KUNA JAMBO LETU LA KATIBA MPYA…

    MHE. KULE ULIKOOA HUKUWAELEWA WANATAKA UWE WAZIRI MKUU AJAE…

    ULIKOOA ULIPELEKA NYOTA YA WATU KUSHINDA BIKO KILA SIKU….

    MHE.. KULE ULIKOOA WAMEPEWA KAZI YA KUTULETEA RAIS WA KWANZA MLEMAVU/KUTOKA UPINZANI

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

Sekta ya Mawasiliano imekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi nchini-Mohamed

Spread the loveWaziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali Mapinduzi Zanzibar Khalid...

HabariHabari Mchanganyiko

TCRA yawataka wasafirishaji wa vipeto kujisajili na wengine kuhuisha leseni

Spread the loveMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa wito...

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

error: Content is protected !!