December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shahidi: Sina mahaba na Mbowe

Spread the love

SHABANI Hassani  Shahidi kwenye kesi namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabali viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameweka wazi kuwa hana mahaba na Freeman Mbowe. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Freeman Mbowe mshitakiwa namba moja kwenye kesi hiyo ni mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni pamoja na Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Zanzibar, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Bara.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini. 

Yafuatayo ni mwendelezo wa mahojiano kati ya Wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala na shahidi huyo.

Kibatala: Ulielekezwa kuonesha hao viongozi uliowataja?

Shahidi: Sikuwataja

Kibatala: Unasema Moshi ulisoma shule gani?

Shahidi: Msasani Sekondari.

Kibatala: Mwalimu wako wa Biology anaitwa nani?

Shahidi: Madamu Tea

Kibatala: Mwalimu wako wa Mathematics.

Shahidi: Abasi.

Kibatala: Jina la pili la Madam Tea.

Shahidi: Alikuwa hana jina.

Kibatala: Namba yako ya mtihani.

Shahidi: 27.

Kibatala: Wakati unasema ulisoma Msasani, nilikuwa ‘nagoogle’ hapa PS/007. Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Necta namba tambuzi ya Msasani ni tambuzi F3371.

Kibatala: Ufaulu wako.

Shahidi; Four ya 30.

Kibatala: Kwa ushahidi wako na utambuzi wako mtu aliyepata four ya 30 anastahili kwenda form five? Unasema namba yako ilikuwa ngapi, 27? Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Necta, mtu mwenye namba hiyo S771/27 alikuwa mwanamke.

Wakili wa Serikali-Kadushi aliingilia kati na kusema: Wakili akiwa anatumia doccument kwa njia ya yoyote lazima aoneshwe na shahidi asije wakili akawa anaongopa na shahidi anasema kweli.

Mawakili wa pande zote mbili wanaingia kwenye mjadala juu ya kifungu alichotumia Wakili Kadushi alikitaja kifungu 154 cha ushahidi.

Hakimu Simba amesema kuwa, matumizi ya kifungu hiko yamekosewa, amemruhusu Wakili Kibatala aendele.

Kibatala: Mwanafunzi mwenye utambulisho S3371/0027 huo uliotaja ni mwanamke?

Shahidi: Ndio namba yangu niliyopewa kwenye mtandao.

Kibatala: Wewe Female au Male?

Shahidi: Male

Kibatala: Kwa mujibu wa tovuti hiyo alipata daraja la 3, wewe kweli ulipata daraja la 3?

Shahidi: 30.

Kibatala: Shahidi somo la Civics ulipata alama gani?

Shahidi: Sijafuatilia.

Kibatala: Ulipata alama gani kwenye somo la Historia?

Shahidi: Sijafuatilia

Kibatala: Unasema unaishi Kinondoni Moscow, pale kuna viongozi wa CCM tutajie kiongozi wako wa CCM pale Moscow.

Shahidi: Mkemimi

Kibatala: Huyu Mkemimi ni kiongozi wa level gani?

Shahidi: Tawi.

Kibatala: Alichaguliwa lini.

Shahidi: Mimi nimemkuta tayari kashachaguliwa

Kibatala:Unamfahamu kiongozi wa Chadema katika eneo unaloishi?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Kiongozi wa TLP?

Shahidi: Siwafahamu siwafuatilii.

Kibatala: Unakitambulisho cha aina gani?

Shahidi: Ninacho cha shule.

Kibatala: Kitambulisho chako cha shule kikowapi?

Shahidi: Moshi.

Kibatala: Kama huna kitambulisho tutajueje kama wewe ndio Shabani?

Shahidi: Nyumbani. Utaenda kuulizia

Kibatala: Unasema siku ya pili baada ya tukio ulipigiwa simu na Polisi hizo namba za simu ulizitaja mahakamani?

Shahidi: Sijazitaja.

Kibatala:Unafahamu kuwa namba za simu lazima zisajili kwa mujibu wa sheria?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Unafahamu kuwa namba za simu sharti zisajiliwe kwa jina la mtumiaji wa simu na zisijaliwe kwa kitambulisho rasmi.

Kama wewe huna kitambulisho na unamiliki simu uliwezaje kusajili line?

Shahidi: Dada yangu ndio aliyenisajili.

Kibatala: Ulimtaja majina dada yako.

Kitambulisho cha Dada yako umekitoa mahakamani.

Shahidi: ndio

Kibatala: Unasema ulipokuwa Moshi ulifaulu na ukasema ulikuja lini Dar es Salaam?

Shahidi: Mwishoni mwa mwezi wa 12 mwaka 2017.

Kibatala: Mtihani wa Form Four uliufanya mwaka gani 2017?

Shahidi: Mwezi wa 11.

Kibatala: Wakati unakuja Dar es Salaam ulishapata kujua kuwa umechaguliwa kuingia kidato cha tano tusaidie matokeo ya Form four yanatoka mwezi gani.

Shahidi: Mwezi wa 12 mwishoni.

Kibatala: Matokeo yako yalitoka mwezi 12 tarehe ngapi?

Shahidi: Yalitoka mwezi wa kwanza.

Kibatala: Ulisema mwezi wa 12?

Shahidi:Mwezi wa kwanza.

Kibatala:Wakati unakuja Dar es Salaan ulisema tayari ulishajua matokeo yako wakati unakuja Dar es Salaam ilikuwa tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 1.

Kibatala: Mwezi wa ngapi?

Shahidi: Wa kwanza.

Kibatala:Dada yako anafanya kazi gani?

Shahidi: Anauza maandazi.

Kibatala: Na mume wa dada yako anafanya kazi gani.

Shahidi: Sijamkuta kashakufa zamani.

Kibatala: Uliongozwa kumtaja mume wa dada yako.

Shahidi: Ndio. Subiri kidogo huyu sio yule ninayeishi naye ninayeishi naye.

Kibatala: Dada yako uliyeongozwa ulimtaja  anaitwa nani?

Shahidi: Mariam.

Kibatala: Ana mume au hana mume.

Shahidi: Anaye.

Kibatala: Uliongozwa kutaja majina yake na anaitwa nani?

Kibatala: Anaitwa Haji Ramadhani.

Kibatala: Anafanya kazi gani.

Shahidi: Mwanamuziki.

Kibatala: Mafunzo ya uchomeaji ulianza tarehe ngapi mwaka gani?

Shahidi: Sikumbuki tarehe lakini ilikuwa mwaka 2017.

Kibatala: Mafunzo uliyaanza mwezi gani?

Shahidi: Mwezi wa 12.

Kibatala: Twende kwa mtu wako uliyemuita boss wako anaitwaje.

Shahidi: Seba.

Kibatala: Uliongozwa kumtaja, huyu Sebeni sebastiana au?

Shahidi: Sebastian.

Kibatala: Anakaa wapi?

Shahidi: Mwanzo alikuwa anakaa Kinondoni sasa hivi anaishi Kibaha.

Kibatala: Umemuona hapa Mahakamani.

Shahidi: Sijamuona.

Kibatala: Yupo hai?

Shahidi: Yupo hadi sasa hivi.

Kibatala: Kinondoni Mkwajuni kuna barabara ngapi.

Shahidi: Zipo nne.

Kibatala: Zitaje.

Shahidi: Zile za kutembea kwa miguu na magari, nilisahau na Barabara Mwendokasi.

Kibatala: Ulikumbuka kuitaka hii barabara ya Mwendokasi au tukio lolote lilitokea kwenye mwendokasi.

Shahidi: Sikuitaja.

Kibatala: Wakati haya yanatokea magari ya mwendokasi yalipita au?

Shahidi: Lilipita moja kabla ya kutokea watu.

Kibatala:Uliiona gari likisimama?

Shahidi: Ndio wakati watu walioingia barabarani.

Kibatala: Hii gari ya Polisi uliyosema ilikuwa ikitoa tangazo ilipita wapi?

Shahidi: Kwenye barabara ya mwendokasi.

Kibatala: Ilikuwa inaaskari wangapi?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Huyu aliyekuwa anatangaza ulimuona.

Shahidi: Ndio nilimuona ila simjui jina?

Kibatala: Huyo askari alikuwa wapi?

Shahidi: Alisimama kwenye mwendokasi.

Kibatala: Wakati hilo gari la Polisi liliposimama basi la mwendokasi liliweza kupita?

Shahidi: Alikuwa anaweza kupita.

Kibatala: Kwamba basi la Polisi limesimama upande fulani basi la Mwendokasi lingeweza kuendelea na Safari zake hilo gari la Polisi lipikuwa halizui?

Shahidi: Lilikuwa halizui.

Kibatala: Ni sahihi kwamba dereva wa gari la Polisi alikuwa makini kiasi ambacho gari la Mwendokasi lingeweza kupita bila wasiwasi.

Hebu tuambia mabomu yalianza kupigwa upande gani?

Shahidi: Kabla ya mtelemko wa bonde la Mkwajuni ndio mabomu yaliyokuwa yakipigwa.

Kibatala: Na hawa watu uliodai wameandamana walikuwa eneo gani?

Shahidi: Walikuwa kwenye barabara zote?

Kibatala:Ni risasi ngapi zilipigwa pale shahidi?

Shahidi: Sijui maana nilikimbia.

Kibatala: Risasi zilipigwa au hazikupigwa?

Shahidi: Mimi nilishakimbia sijui lakini mabomu yalipigwa.

Kibatala: Ulikimbia umbali gani.

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Ulisikia sauti ya risasi hukusikia?

Shahidi: Sijasikia maana nilikuwa nishaondoka.

Kibatala: Ulitaka majina ya maduka ya watu ulitaja Meredian Bet mwenye hii Meridian Bet unamfahamu?

Shahidi: Simfahamu.

Kibatala: Linafanya kazi au haifanyi kazi?

Shahidi: Linafanya kazi.

Kibatala: Maduka yote yanafanya kazi hayafanyi kazi.

Kibatala: Ulisema saa saba ulikwenda kwenye sala uliongozwa kusema chochote?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Unasema ulipotoka baada ulipangiwa kazi na boso wako na alikuita wewe na watu wengine?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Nilikuelewa vizuri kwamba hili duka lenu lipo pembezoni mwa barabara?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Ni sahihi hawa wafanyakazi wengine waliobaki pale maana wewe ulipewa kazi ya kununua flat Bar hawa wafanyakazi wenzako wengine walienda wapi, Ni sahihi kwamba wenzako hawakupewa majukumu ya kuondoka baada ya wewe kuondoka?

Shahidi: Mimi nilipopewa hela niliondoka wao sijajua walipewa kazi gani.

Kibatala: Nifafanulie wakati unatoka kuswali uliwepewa hela na kupewa jukumu?

Shahidi: Mimi nilipewa jukumu la kwenda kununua Flat bar na Stiki

Kibatala: Na kwa ufahamu wako hadi watu wa Chadema kutokea duka lilikuwa limefungwa au bado?

Shahidi: Lilikuwa halijafungwa.

Kibatala: Na uliacha watu wote pale?

Shahidi: Niliacha watu wote pale.

Kibatala: Hawa wenzako ukiomtoa Seba mpo wangapi?

Shahidi: Tupo watano.

Kibatala:Hawa wanne wengine uliwataja majina?

Shahidi: Sikuwataja.

Kibatala: Ulivyorudi saa moja ulikuta duka lenu lipo wazi limefungwa.

Shahidi: Nilikuta limefungwa niliingia kwa nyuma.

Kibatala: Na huwa mnafunga saa ngapi?

Shahidi: Saa mbili

Kibatala: Huo mlango wa nyuma ni geti la nyumba au kuna baadhi ya nyumba zina maduka mbele yake?

Shahidi: lipo kwenye Ofisi za CCM pale.

Kibatala: Ofisi za CCM zipo wapi?

Shahidi: Mkwajuni.

Kibatala: Hawa wenzako walikuwa wapi.

Shahidi: Walikuwa wapo wametulia wananyoosha nguo zao wakinisubiri mimi nirudi.

Kibatala: Ulikiona kitambaa gani wakati gari la Polisi likitoa amri ya kutawanyika?

Shahidi: Chekundu.

Kibatala: Hawa watu waliokuwa wakija uliweza kufahamu walipata madhira gani huko walipotokea?

Shahidi: Sijui walipotokea.

Kibatala: Ulisema Bosi wako alikupa hela na ukaenda nazo dukani mkiwa pale mnapigiana mahesabu ndio mkaona zogo linatokea kwa mbali uliongozwa kusema chochote kuhusu hizo hela?

Shahidi: Hela niliziacha kwa mwenye duka nikamwambia nitazifuata kesho.

Kibatala: Na hivyo vifaa vya welding.

Shahidi: Nilivifuata kesho.

Kibatala: Kwa hiyo hela la vifaa vilikuwa salama?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Ulikimbia baada ya kuona watu au mabomu?

Shahidi: Baada ya mabomu.

Kibatala: Na huyu mwenye duka alifunga baada ya mabomu au hawa watu?

Shahidi: Alifunga baada ya kuona kundi la watu.

Kibatala: Na huyo Baba John alikuambia alifunga duka kwa sababu gani?

Shahidi: Alifunga duka baada ya kuona wale watu na askari kuwa mbele ya wale watu akasema ngoja nifunge duka.

Kibatala: Ulisema walirusha maji mawe na miti uliongozwa kusema hivi vitu vilirushwa na fulani ambaye yupo hapa mahakamani?

Shahidi: Sikuongozwa.

Baada ya kumaliza Kibatala alimwachia Wakili Profesa Safari pamoja na John Mallya kwa ajili ya kuendelea kumhoji shahidi.

Mallya: Shahidi kati ya dada yako na bosi wako nani alitangulia kujiunga na CCM?

Shahidi: Dada yangu ni Chadema, Bosi wangu sijui chama gani.

Mallya: Tuambie sababu inayokufanya usijue matokeo yako ya Civics na kumjua kiongozi wa Moscow unapoishi?

Shahidi: Matokeo sijafuatilia, niliambiwa na wenzangu. Kiongozi wa CCM nakaa naye nyumbani, tumezoeana.

Mallya: Uliulizwa wakati unaongozwa kuwa hiyo hali iliwaona nayo hao watu ilikuwa  ni shari, nini kilichokufanya useme hiyo hali ni shari wimbo zao.

Shahidi: Wimbo zao na jinsi walivyo.

Mallya: Nyimbo gani?

Shahidi: Watatuua hatupo.

Mallya: Kwa hiyo nikisema utaniuwa ni shari?

Shahidi: Inategemea

Mallya: Hivi mimi na wewe tunaongea, nikasema wewe na Kadushi mtaniua ni shari?

Shahidi: Sio shari

Mallya: Wimbo mwingine ni wimbo gani?

Shahidi: Hatupoi

Mallya: Sasa mimi na Kibatala na Nchimbi tumeongozana, tunasema hatupoi, inakuwa shari?

Shahidi: Inategemea na mazingira.

Mallya: Shahidi nyimbo ya hatupoi tupo mia moja, tunaimba tunaimba hatupoi, hiyo inakuwa shari?

Shahidi: Kwa upeo wangu mimi ni shari. Inategemea na mlivyo kwa wakati huo mnaweza mkawa mnacheka au mmenuna, nitajua hawa jamaa wamekasirika.

Mallya: Uliongozwa kusema kuwa, hao watu walikuwa wamenunua au wanacheka?

Shahidi: Sikuulizwa

Mallya: Shahidi ilikuwa ni mara yako ya kwanza kuona watu wapo katika hali hiyo?

Shahidi: Sio mara ya kwanza?

Mallya: Kabla ya tarehe 16, ushawahi kuona hali hiyo labda wamasai wameshika fimbo kule Moshi?

Shahidi: Niliwaona wameshika, mtu kashika fimbo.

Mallya: Uliwaona watu wameshika fimbo na kusababisha watu kufunga maduka?

Shahidi: Sasa mmasai kushika fimbo utafungaje maduka?

Mallya: Hao watu waliofunga maduka walikuambia walifunga maduka kwa sababu gani?

Shahidi: Sikuwa nao mimi, nilikuwa na mtu mmoja tu.

Mallya: Kwa hiyo hawa waandamanaji walikuwa hapo Mkwajuni, ilikuwa saa ngapi?

Shahidi: Saa 11 kuelekea saa 12

Mallya: Nimezungumza kuhusiana na gari la polisi lilikuwa likikatisha katika ya waandamaji, lilikuwa likitembea spidi gani?

Shahidi:  Taratibu sana

Mallya: Kwa kukadiria umbali wa askari na waandamaji.

Shahidi: Kutoka kwenye ukuta hadi hapa ulipo wewe (ukuta wa mahakama).

Mallya: Kutoka hapa niliposimama inaweza kuwa mita ngapi? Unatumia futi umesema futi yako inafuti ngapi?

Shahidi: 360

Mallya: Inaweza kufika wapi hapa tulipo?

Shahidi: Hapo hadi kwenye hilo benchi (ndani ya mahakama).

Mallya: Kwa hiyo futi yako ikifika hadi kwenye ukuta, itakuwa umbali gani?

Shahidi: Futi 460

Mallya: Ambayo ndio usawa wa waandamanaji na askari?

Shahidi: Ndio

Mallya: Akwelin alikufa kwenye tukio hilo, alikuwa kwenye gari gani?

Shahidi: Sijui

Mallya: Unakumbuka mara ya kwanza unakuja Dar es Saam ilikuwa lini?

Shahidi: Mwezi wa 12 mwaka 2017

Prof Safari akamuhoji shahidi: Ulisema ulipewa hela ya kwenda kununua vifaa, kiasi gani ulipewa?

Shahidi: 130,000.

Prof Safari: Ulisema askari walivyofika kwenye eneo hilo, walikuja na wakasema maneno gani?

Shahidi: Watawanyike

Prof Safari: Kuna shahidi alisema alitamka neno Ilani, ulisikia?

Shahidi: Sijasikia

Prof Safari: Una mahaba na Mbowe? Unampenda Freeman Mbowe?

Shahidi: Sina mahaba naye sana

Prof Safari: Mbowe humpendi, je Halima Mdee unampenda au humpenda?

Shahidi: Halima Mdee nampenda

Prof Safari: Kwanini unampenda Halima Mdee?

Shahidi: Jinsi maongezi yake bungeni

Prof Safari: Na kwanini humpendi Mbowe?

Shahidi: Simfuatilii sana

Prof Safari: Je Matiko unapenda au humpendi?

Shahidi: Simfuatili

Prof Safari: Je unamjua Makonda, unampenda au humpendi?

Shahidi: Kwa vile ndio mkuu wetu wa mkoa, nalazimika kumpenda

Prof Safari: Wewe ulipata division four halafu umemwambia hakimu ulifaulu kwenda kidato cha tano.

Shahidi: Kwa nini?

Prof Safari: Kwa jinsi nilivyoambiwa. Unalala wapi wewe?

Shahidi: Nyumbani

Prof Safari: Kwa nani?

Shahidi: Dada yangu.

Prof Safari: Uliandika maelezo Osterbay?

Shahidi: Ndio

Prof Safari: Yako wapi?

Shahidi: Sijui

Prof Safari: Ulipenda kutoa ushahidi mahakamani?

Shahidi: Nilipenda

Prof Safari: Kwahiyo unaona raha sana?

Shahidi: Hamna, niliambiwa na askari.

Prof Safari: Alikuambiaje?

Shahidi: Nije mahakamani kutoa ushahidi

Baada ya hapo alihitimisha wakili wa Serikali Kadushi kwa kufanya masahihisho juu ya maswali aliyoulizwa shahidi wa kesi hiyo.

Kadushi: Shahidi nitakuuliza maswali machache kwa ajili ya ufafanuzi.

Nitakuuliza kuhusu namba ya usajili matokeo yako ya mtihani mpaka wakili alipokuwa akikuuliza alikuwa ‘a’ nawe unajibu ‘b’. Alikuwa akikuuliza kwenye nini.

Shahidi: Simu

Kadushi: Ya nani?

Shahidi: Sijajua kama yake au vipi.

Kadushi: Namba za shule alikuwa akikuuliza kwenye nini?

Shahidi: Simu.

Kadushi: Mtandao gani aliokuwa akitumia kukulizia namba yako?

Shahidi: Sijui.

Kadushi: Nafasi gani ulipata kujua simu hiyo wewe au mahakamani.

Shahidi: Sijapata nafasi.

Kadushi: Na Muheshimiwa Hakimu au Mahakama?

Shahidi: Haikupata nafasi ya kuangalia.

Kadushi: Kuhusiana na matokeo yako mojamoja ulimjbu nini?

Shahidi: Nilimjibu sijui.

Kadushi: Matokeo ulitaka moja moja au katika muktadha gani?

Shahidi: Nilitaja yote.

Upande wa Serikali ukamaliza kumuuliza shahidi huyo wa mwisho na kwamba leo itamfikisha mahakamani shahidi wa tatu.

Hakimu Simba ameiahilisha kesi hiyo mpaka leo saa tatu asubuhi.

error: Content is protected !!