Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Shahidi: Maandamano Chadema zilipigwa zaidi ya risasi 90, Akwilina atajwa
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Shahidi: Maandamano Chadema zilipigwa zaidi ya risasi 90, Akwilina atajwa

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kusutu imeendelea na usikilizaji wa kesi inayowakbali viongozi Waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo leo tarehe 13 Mei upande wa utetezi uliendelea kumhoji shahidi wa Serikali juu ya ushahidi wake, Ananripoti Faki Sosi …(endelea)

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba shahidi  wa Jamhuri Gerlad Ngichi ambaye ni Mkuu wa Operesheni jeshi la Polisi Mko wa Kinondoni amehojiwa na jopo la mawakili wa utetezi liliongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Hekima Mwasibu, na Jeremiah Mtobesya na John Mallya.

Huku wakili wa serikali ukiongozwa na Faraja Nchimbi sambamba na Paul Kadushi.

Wakili Kibatala aliendelea na maswali kwa shahidi SSP Gerald Ngichi.

Kibatala: Mara ya mwisho wakati unatoa ushahidi wako ulisema kuna watoto na wazee walipotea mueleze hakimu jinsi wazee na watoto hawa walivyoonganishwa na familia zao na kama ulisema chochote juu hilo?

Shahidi: Nilisema.

Kibatala: Mueleze Hakimu  watoto na wazee hao waliunganishwa kwa namna gani na familia zao?

Shahidi: Baada ya  kuripotiwa kuripoti kwao sisi tuliwapeleka kwenye vituo vya karibu na familia zao.

Kibatala: Ulitaja majina ya hao ndugu?

Shahidi: Sikutaja.

Kibatala: Shahidi nilikusikia ukitoa ushahidi kuwa pale eneo la tukio walikamatwa watuhumiwa makundi mawili, washtakiwa na pamoja na watu wengine ambao mimi nafikiri kuwa ni watuhumiwa ulisema chochote kwenye ushahidi wako kuhusu hawa watu wengine?

Shahidi: Nilisema tuliwakamata watuhumiwa 43.

Kibatala: Na hatua gani walichukuliwa hao watumiwa wengine .

Shahidi: Walipelekwa kituo cha Polisi cha Osterbay.

Kibatala: Na baada ya hapo walisamehewa kwa hisani ya Polisi.

Shahidi: Upepelezi siufahamu.

Kibatala: Wewe unaufahamu binafsi kilichowatokea hawa watuhumiwa wengine 43 uliosema umewakamata, juu ya kufunguliwa kesi.

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Ulisema chochote juu ya kufunguliwa kesi kwa hawa watuhumiwa .

Shahidi: Ndio walifynguliwa kesi Polisi Osterbay

Kibatala: Ulitaja majina hao watuhumiwa mahakamani?

Shahidi:Hapana.

Kibatala: Wakati unatoa ushahidi wako ulisema kuwa Mbowe alitimua mbio na kwamba hukuwahi kuona akitimua mbio namna ile na ulisema alidondosha miwani sahihi?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Iyo miwani iko wapi?

Shahidi Sijui.

Kibatala: Ni sahihi eidha wewe au askari wako walichukua mawani hiyo kama ushahidi?

Shahidi: Alichukua mwenyewe.

Kibatala: Kwa hiyo mtu alitimua mbio alirejea kuokota miwani.

Kibatala: Ulisema chochote kuhusu mavazi?

Shahidi: Sikusema.

Kibatala: Freeman Mbowe Alikamatwa eneo la tukio au eneo lolote linalohusiana na tukio?

Shahidi: Alikamatwa nyumbani.

Kibatala: Ulisema unaskari wangapi?

Shahidi: Zaidi ya Hamsini

Kibatala: Lakini hakuna askari hata mmoja aliyemkata Mbowe?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Ni mtuhumiwa gani muliyemkata eneo la tukio?

Shahidi: Hakuna.

Kibatala: Mulirekodi ushahidi wowote ?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Vifaa vya kurekodia alikuwa navyo nani?

Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Kinondoni na Wilaya

Kibatala: Hawa maofisa walikuwepo eneo la tukio?

Shahidi: Timu zao zilikuwepo.

Kibatala: Wao wenyewe walikuwepo hawakuwepo?

Shahidi: Hawakuwepo.

Kibatala: Unaufahamu binafsi namna maofisa hawa walivyotoa vifaa hivi vya kurekodia?

Shahidi: Wao ndio wanajua jinsi ya kutoa vifaa vya kazi?

Kibatala: Wakati washtakiwa wanahojiwa ulikuwepo na unafahamu chochote juu ya kile walichihojiwa?

Shahidi: Sikuwepo.

Kibatala: Unafahamu  kuwa Ester Matiko wakato watuhumiwa wanahojiwa alikuwepo Tarime akifanya Mkutano kama mbunge aliopewa kibali na jeshi la Polisi?

Shahidi: Hayanihusu.

Kibatala: Unafahamu kuwa Msigwa mara tu baada ya Mkutano kuisha alianza safari ya kwenda Iringa?

Shahidi: Ninafahamu kuwa hakuondoka ndio maana alikuwepo kwenye maandamano.

Kibatala: Unasema pia Freeman Mbowe aliondolewa kwenye Mkutano na walinzi wa Mbowe kwa maoni yangu mimi walichokifanya walinzi wa Mbowe pia ni kosa la Jinai mwambie Hakimu kama muliwakamata?

Shahidi: Nilishakueleza kuwa watuhumiwa walipelekwa Polisi.

Kibatala: Hao walinzi uliwakamata?

Shahidi: Nilishajibu kati ya hao watu 43 niliwakamata kama walikuwemo niliwakamata.

Kibatala: Katika shitaka la Kwanza watuhumiwa walikula njama kufanya kosa la kusanyiko kinyume na sheria mueleze Hakimu walikutana wapi?

Shahidi: Sijui walipokutana.

Kibatala: Shitaka la Pili walifanya kosanyika lisilo halali kuanzia uwanja wa Buibui. Nataka kujua walipokuwepo Buibui walikuwa kisheria?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Mwambia Hakimu kwamba uwepo wa watuhumiwa Buibui kama walikuwa sawa kisheria?

Shahidi: Walikuwa sawa kisheria kwa sababu walikuwa wafunga kampeni.

Kibatala:  Kwenye Shitaka la nne ni Mbowe alisema maneno hayo “hapa napozungumza kiongozi wa Hananasifu yupo Mortuary(chumba kuhifadhi maiti) ni kweli wakati anahutunia maneno hayo kulikuwa na Kiongozi alikuwa Mortuary?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Alifikaje hapo ‘Mortuary’?

Shahidi: Kwa kawaida maiti huwa anahifadhiwa Mortuary kusubiri maziko au upelelezi?

Kibatala: Nini chanzo cha kifo cha huyo kiongozi wa Hananasif?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Alinyongwa na kuuawa.

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Mbowe alisema halafu siye tunaona kawaida.Kunyongwa hadi kuuawa ni jambo la kawaida kawaida?

Shahidi: Sio kawaida

Kibatala: Mbowqe alisema pia kwa mujibu wa hati ya mashtaka “Hiko kimempata marehemu halafu Tunacheka na Polisi uliweza kufahamu alikuwa akilenga nini?

Shahidi: Nifahamu akimaanisha nini.

Kibatala: Bila shaka pia ufahamu aliposema tunacheka na CCM alimaanisha nini?

Kibatala: Haya maneno uliyasikia binafsi au kuna mtu alikusimulia.

Shahidi: Sijayasikia

Kibatala: Shitaka la sita linasema kuwa alifanya uchochezi wa Uasi. Mbowe alisema “Tumejipa kibali cha kutangulia mbele ya haki” wewe unafahamu alilenga ninu hapa?

Shahidi: Kutangulia mbele ya haki ni kufa.

Kibatala: Kwani mwisho wa siku Mbowe atakufa au hafi?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Maneno mengine amesema kuwa haiwezekani wanaume wazima kama sisi tufanywe mandondocha kwani kuna tatizo gani kwenye maneno haya Mwanaume mwenye watoto  na mke  kama Mbowe kukataa kufanywa ndondocha?

Shahidi: Sijui?

Kibatala: Maneno mengine mbowe alisema “Mimi nipo hapa kuliandaa taifa kunatatizo gani Mbowe kuliandaa taifa?

Shahidi: Inategemea kwa namna gani anataka kulianda taifa?

Kibatala: Juzi Jacob Zuma alilazimishwa kujiuzulu ni kweli Zuma alilazimisha kujiuzulu?

Shahidi: Kweli

Kibatala: Mbowe alisema Mugabe Kang’olewa ni kweli Mugabe Kang’olewa?

Shahidi: kweli

Kibatala: Alisema  Magufuli ni mwepesi kama karatasi wewe unaufahamu uzito wa Magufuli?

Shahidi: Magufuli ni nani sijakuelewa.

Kibatala: Magufuli aliyeandikwa kwenye hati ya Mashtaka?

Shahidi: Anamfahamu aliyeandika hati ya mashtaka.

Kibatala: Shitaka la saba Mdee alichochea uasi alisema alisema “sihitaju kuelezea madhira” . Unayafahamu hayo madhira?

Shahidi: Mimi sikuwepo wakati anazungumza hayo maneno.

Kibatala: Kuna maneno mengine kwamba “kesho tukamchinje Magufuli na vibaraka wake wote” ulifanikiwa kufahamu kuwa kumchinja kwa maana ya uchaguzi kutimchagua yeye na watu wa chama chake?

Shahidi: Sijamsikia.

Kibatala: Shitaka la nane linamuhusu Heche  kwanza ni sahihi kuwa tarehe 17 Februali 2018 kuwa kulikuwa na zoezi uchaguzi jimbo la Kinondoni?

Shahidi: Siku inayofuata baada ya Kampeni ndio ilikuwa  siku ya uchaguzi.

Kibatala: Heche alisema Kesho patachimbika upumbavu uliofanya kwenye nchini hii” wewe unafahamu kuwa alimanisha (kui-vote out CCM)?

Shahidi: Siijui maana sikuwepo.

Kibatala: Hili suala kuwa watu wanapotea ni kweli au sio kweli?

Ni kweli kwamba kuna watu wanapotea na Jeshi la Polisi halijui walipo?

Shahidi: Watu wanaopotea wanaripotiwa Polisi.

Kibatala: Kuna Mwandishi wa Habari amepotea anaitwa Azory Gwanda? unafahamu.

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Kuna Mtu anaitwa Ben Saanane unafahamu alipo na nini kimemtokea ?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Kama wewe hujui hawa watu wawili wamepotea yeye akisema kuna watu wamepotea kisheria tatizo liko wapi?

Shahidi: Kama imeripotiwa Polisi wanafuatilia

Kibatala: Watu wanauwa na wanaokotwa kwenye mitaro ni kweli kwamba watu wanauwa wanaokotwa kwenye mitaro?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Mbowe alisema nitaongoza mapambano najua watu watakao kufa watalea haki kwenye nchi hii ni kweli ulisikia mshatiwa wa kwanza alisema mameno hayo?

Shahidi: Sikusikia

Kibatala: Shtaka la 11Mbowe aliwachochea wakazi wa Kinondoni je unawajua kwa majina hao wakazi?

Shahidi: Siwafahamu hao wakazi kwa kuwa sikuwepo aliposema.

Kibatala: Shahidi shtaka 12 linamuhusu Peter Msigwa

Mshtakiwa aliwachochea wakazi wa kinonondoni wabebe silaha ulisikia akisema maneno hayo?

Shahidi: Sikuwepo

Kibatala: Shtaka la 13 Bulaya aliwachochea wananchi wa Kinondoni kujilinda ili kupatikana kwa haki, ulimsikia?

Shahidi:Sikumsikia

Kibatala: Shahidi ni nani sasa hasa alisikia hayo maneno?

Shahidi: Maofisa ya jeshi la polisi waliokuwa wakisimamia mkutano wa kufunga kampeni

Kibatala: Wakati nakuuliza awali kuhusiano na uchukuaji wa video ulionyesha kutokuwa na ufahamu binafsi na lakini ulipokuwa barabara ya  kawawa ulipokuwepo uliwai kuonyeahwa video iliyochukuliwa Kawawa?

Shahidi: Sihitaji kukujibu

Hakimu Simba: Jibu

Shahidi: sikuonyeshwa

Wakili Kibatala amemaliza kuuliza maswali kwa shahidi na kumwachia kiongozi wa Jopo Profesa Safari aliyeitambulisha Mahakama kuwa atauliza John Mallya.

Mallya: Shahidi umezaliwa mwaka gani

Shahidi: Nimezaliwa mwaka 1972

Mallya: Unamiaka mingapi?

Shahidi: 47.

Mallya: Wakati unajiunga na Polisi ulikuwa na Miaka mingapi, 2000

Au nikusaidie miaka 28.

Mallya: miaka 28 ulikuwa na Degreee ya Kozi gani?

Shahidi: Sheria.

Mallya: Ulianza mwaka gani.

1996.

Mallya: Kwa mujibu wa PGO ni sahihi kwamba mtu akiwa na miaka 28 haruhusiwi kujiunga na jeshi la Polisi?

Wakili Nchimbi: Mheshimiwa hakimu tujiepushe na maneno ya kumuondolea mtu heshima.

Mallya: Kiwango cha Mwisho cha Umri kujiunga na Polisi.

Shahidi: Inategemea na Elimu .

Mallya: Mimi nina miaka 31 nina degree ya Sheria naruhusiwa kujiunga na Polisi?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Kesi unayoitolea ushahidi unahusiana na maswala ya uchaguzi nyinyi kama wadau mlipewa elimu juu ya usimamizi wa uchaguzi?

Shahidi: Natoa ushahidi juu ya maandamano yasiyo halali.

Mallya: Lakini inatokana na uchaguzi ni kweli si kweli?

Shahidi: Kweli.

Mallya: Mlipewa mafunzao ya kuoata mafunzo mahususi juu ya usimamizi? wa uchaguzi

Shahidi: Jeshi la polisi linamafunzao ya kusimamia chaguzi mablimabali ndogo na kubwa.

Mallya: Shahidi ulizungimza mambo ya ratiba ya kuonyesha mikutano ya kampeni?

Shahidi: Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni na anampa Kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni.

Mallya: Wewe sio kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ni kweli sio kweli?

Shahidi: Kweli.

Mallya: Wewe ulipewa na nani barua ya kuonyesha mikutano ya vyama vya siasa?

Shahidi: Mkuu wa Polisi Kinondoni.

Mallya: Kwa hiyo shahidi mkurugenzi alikuwa anampa RPC na aRPC anakupa wewe?

Mallya: Alikuwa nakupa kwa njia gani mlikuwa mnapeana kienyeji au kwenye korido?

Shahidi: Taribu za jeshi nchi mzima huwa wanapata maelekezo kutoka wa Ma RPC.

Mallya: Utaratibu gani?

Shahidi: Nakuambia kuwa sisi ndio Watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi.

Hakimu Simba: Kadushi muelekeze.

Mallya: Hii barua imefikaje mikononi mwako ?

Shahidi: Vikao vya asubuhi vinaelekeza shughuli za siku mzima mim ndio nilikuwa nina jukumu la kufanyia kazi.

Mallya: Nitakuonesha Sheria ya uchaguzi na nitakulliza fact. Kifungu cha 51 (5) cha Sheria ya Uchaguzi kila Mkuu wa Wilaya anawepa nakala ya ratiba na barua ya kampeni za uchaguzi?

Mallya: Kwa mujibu wa sheria hii hujavunua sheria kupewa barua hii RPC.

Hapajavunja sheria yoyote?

Mallya: Unafahamu vituo vya kupiga kula vilikuwa vingapi?

Shahidi: Vilikuwa vingi sikumbuki idadi yake.

Mallya: Vingi vingapi 200 au 100?

Shahidi: Zaidi ya Hamsini.

Mallya: Umesema unafahamu uwepo wa Mawakala unafahamu huyu wakala anayesimamia uchaguzi lazima awe na kiapo?

Shahidi: Sijafahamu.

Mallya: Ili mtu atambulike kuwa ni wakala awe na nin?

Shahidi: Lazima atambuliwe na Mkurugenzi nwa Manspaa.

Mallya: Mimi Wakala wa Salum Mwalimu  ni sahihi ili Mkurugenzi anitambue mimi anitambulishe kwa Mkurugenzi?

Shahidi: Sawa.

Mallya: Utaratibu wa Mkurugenzi na Mwalimu kuwatambulisha mawakala wake unaufahamu?

Shahidi: Siufahamu.

Mallya: Kwa hiyo hutambui kuwa mwalimu na Mkurugenzi waliambizana wakutane Jioni?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Ili uwe wakala uwe na sifa gani?

Shahidi: Uwe na umri zaidi ya 18 .

Mallya: Unafahamu wakala wa Mwalimu ni Kina nani?

Shahidi: Sijui

Mallya: Unafahamu kuwa Mbowe alikuwa ni wakala?

Shahidi: Sijui

Mallya: Unafahamu kama mshitakiwa wa Pili Peter Msigwa alikuwa ni Wakala?

Shahidi: Sifahamu .

Mallya: Unafahamu mshitakiwa na tano ni Wakala wa Mwalimu?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Kwa hiyo hufahamu kuwa hawa washtakiwa wote ni mawakala?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Ulijihusisha na Uchaguzi unafahamu barua za kuwatambulisha mawakala zinatoka lini?

Shahidi: Sijui.

Mallya: Kwa hiyo ratiba uliyokuwa nayo lakini kunusu mawakala hukujishughulisha?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Ulikuwa na ratiba ya kampeni za door to door (nyumba kwa nyumba) ulikuwa nayo?

Shahidi: Hapana.

Mallya: Kama walikuwa wanavuka barabara ulijuaje kama walikuwa wanafanya kampeni?

Shahidi: Hapana kampeni hazifanyika barabarani.

Mallya: Zinafanyika wapi?

Shahidi: Nyumbani.

Mallya: Ili ufike nyumbani unapita wapi?

Shahidi: Barabarani.

Mallya: Ulisema kwenye maandamano yale kuna waandamanaji walikuwa wanarusha chupa za maji unafahamu kuna mtu anaitwa Akwilina alikufa kwa sababu ya kupigwa chupa?

Shahidi: Sijui.

Mallya: Unasema muliwakamata waandamaji 43 ni mwandamanaji gani alikutwa na risasi?

Shahidi: Hakuna

Mallya: Ulisema kuwa askari wako uliwaamuru warushe risasi hewani walitutumia silaha ya aina gani?

Shahidi: Ak47.

Mallya: Bunduki ya Ak47 risasi yake ikipigwa inaenda wapi?

Shahidi: Inaenda hewani.

Mallya: Inaenda hewani inarudi wapi?

Shahidi: Inarudi chini.

Mallya: Ulikuwa unasimamia Operesheni ulikuwa unajua hizi risasi zinarejea kwenda chini zilikuwa zikienda upande gani?

Shahidi: Ardhini.

Mallya: Upande gani maana nyie mulikuwa mukipiga kuangalina wenyewe au waandamanaji?

Shahidi: Waandamaji.

Mallya: A47 ikitua inatua kwa umbali wa mita ngapi?

Shahidi: Mita nyingi zaidi ya mia 500.

Mallya: Kutoka kituo cha Basi Mkwajuni inakwenda mita 500 mbele?

Shahidi: Hewani.

Mallya: Zinaposhuka chini umbali gani ?

Shahidi: Zinashuka umbali ulioruka.

Mallya: Zinashuka mita 20 au zaidi whetever lakini zinashuka ambapo watu wapo?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Ulisema hawa askari waliokuwa wanarusha risasi walikuwa wangapi?

Shahidi: Watano.

Mallya: Walirusha risasi ngapi?

Shahidi: Zaidi ya 90.Kila askari anapiga kwa kadri anavyoelekezwa wengine tatu wengine nne lakini walipiga zaidi ya 90.

Mallya: Risasi zimepigwa zaidi ya 90 waandamanaji walikuwq zaidi ya 500 hawa waandamani na hawa 43 hakuna aliyeangukiwa na risasi risasi ilimuuangukia nani?

Shahidi: Risasi ikidondoka inakuwa haina madhara.

Mallya: Risasi zilizodondoka zaidi ya 90 uliziokota tuzitumie kama ushahihidi?

Shahidi: Kinachookotwa ni maganda sio risasi.

Mallya: Tukimleta hapa shahidi aliyepepigwa risasi kwenye tukio hilo utasemaje?

Shahidi: Mahakama itaamua.

Mallya: Sababu ya wewe kuzuiya maandamano ni Ofisi za Mkurugenzi kufungwa nyengine ulisema kulikuwa na wagonjwa iambie Mahakama kulikuwa na wagonjwa wangapi?

Shahidi: Sikuwa nahesabu wagonjwa.

Mallya: Ulijuaje kama kuna wagonjwa?.

Shahidi: Njia ile inatumika na amburance kulikuwa Amburance 3 zilizuiwa.

Shahidi: Maandamano chadema zilipigwa zaidi ya risasi 90/ Akwilina atajwa Wewe ulipoulizwa kuhusu Matiko umesema hakuhusu mbona ulimkamata ?

Shahidi: Kwa sababu alikuwepo kwenye mkutano.

Mallya: Mshtakiwa watatu ulisema alikuwa hatembie alikuwa anaandamana unaandamanaji kwenye gari?

Shahidi: Gari lilikuwa la wazi.

Mallya: Mimi sitembei nipo kwenye gari naandamanaje?

Shahidi: Nilisema mkutano huo ulikuwa haramu kwa hiyo mtu yoyote kama alikuwa kwenye gari au kwa miguu ameandamana.

Mallya: Ulisema kuwa mshaitakiwa 7 na 9 Halima Mdee na Bulaya umesema walikuwa wameandamana walivaaje?

Shahidi: Ni muda mrefu umefika sikumbuki simtambui mtuhumiwa kwa sura sio kwa mavazi kwa sababu wengine walivaa njano kama Mbunge wa Kibamba.

Mallya: Unafahamu Mnyika alivaa nguo gani?

Shahidi: Kama nilivyokujibu nakujibu jumla.

Mallya: Sitaki majibu ya jumla?

Shahidi: Sikumbuki.

Mallya: Unaweza kuyataja majina ya walinzi wa Mbowe ulioseme kwenye ushahidi wako kuwa waliomtorosha?

Shahidi: Siwezi kuyajua.

Mallya: Ulijuaje kama walinzi wa Mbowe ?

Shahidi: Walikuwa karibu na Mbowe.

Mallya: Heche alikuwa karibu na Mbowe naye Mlinzi wa Mbowe ?

Shahidi: Walikuwa mstari wa mbele wote.

Mallya: Unafahamu Wilaya ya Kinondoni inamajimbo mangapi?

Shahidi: Mawili.

Mallya: Mkoa wa Polisi wa Kinondoni una wilaya ngapi?

Shahidi: Tano.

Mallya: Moja wapo wilaya ya Kinondoni ?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Ni sahihi kuwa kila wilaya ina OCD wake?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Kila OCD anaongoza wilaya yake bila kuingiliwa na Wilaya nyengine?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Kwa hiyo Mkurugenzi wa Uchaguzi akimkopi RPC anawajibu wa kumnukuu OCD wa Wilaya Nyengine?

Shahidi: Ndio.

Mallya: Ratiba ya Kampeni iliyotumwa na Mkurugenzi kwenda kwa OCD wa Kinondoni aliwaruhusu wafanye maandamano?

Shahidi: Sio kweli.

Mallya: Wewe ni OCD wa Kinondoni?

Shahidi: Hapana.

Mallya: Shahidi unafahamu kwamba taratibu za uchaguzi kuna kamati inashughulika na migogoro ya kampeni ?

Shahidi: Sifahamu.

Mallya: Kwenye mkutano wa Chadema ulisema watu walikuwa wangapi kwa makadirio yako?

Shahidi: Mimi sikuwepo kwenye mkutano. Nilikagua na kuondoka.

Mallya: Wakati unakagua kulikuwa na watu wangapi kwa makadirio ?

Mallya: 200 na wengine wakiongozeka.

Mallya: Wakati unakagua watu zaidi ya 200 ulipata nafasi ya kupanga hawa waondokeja?

Shahidi: Sio kazi yangu.

Mallya: Ni sahihi kwamba hawa watu ni wakazi wa Jimbo la Kinondoni?

Shahidi: Sahihi.

Mallya: Ulipata kufahamu hawa watu 200 wanakaa nyumbani ?

Shahidi: Sikuulizia.

Mallya: Hawa watu 200 Wakati wanakuja ulijua wanatoka eneo gani na walifikaje pale?

Shahidi: Watu wametembea wengine kwa pikipiki wengene magari kutegemea na umbali.

Mallya: Hawa watu walikuja na miguu bajaji pikipiki.Wakitembea hawajakosea?

Shahidi: Hawajakosea.

Mallya: Wakipanda pikipiki?

Shahidi: Hawajakosea.

Mallya: Ushawahi kusimamia mtanange wa kwenye uwanja wa Mpira kiwanja cha Taifa simba na yanga?

Shahidi: Sio Wilaya yangu.

Mallya: Umewahi kusimamia popote suala la kiusalama kwenye suala la michezo?

Shahidi: Hapana.

Mallya: Kwa uelewa wako mtu akisema leo simba itaichinja yanga wewe unaelewaje .

Shahidi: Inategemea anazungumzia wapi?

Mallya: Uwanjani

Shahidi: Inamaana wataifunga.

Mallya: Wakisema kwenye uchaguzi Chadema wataichinja CCM?

Shahidi: Inamaana wataishinda.

Itaendelea….

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

error: Content is protected !!