Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi kesi ya Zitto amtaja Lissu
Habari za Siasa

Shahidi kesi ya Zitto amtaja Lissu

Spread the love
SHAHIDI wa tatu, Shabani Hamis (40) kwenye kesi  Na. 327/2018 ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameieleza mahakama kwamba, tukio la kushambuliwa Tundu Lissu limefanya azidi kulichukia Jeshi la Polisi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alishambulia na watu wasiojulikana tarehe 7 Septemba 2017 Area D, jijini Dodoma.
Jana tarehe 16 Mei 2019, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya Zitto ambapo upande wa Jamhuri ulipeleka shahidi wao wa tatu (Hamis) ambaye alitoa ushuhuda wake juu ya kesi hiyo.
Upande wa Serikali kwenye kesi hiyo uliongozwa na Wakili Mkuu, Tumaini Kweka, Nassoro Kadushi na kwa upande wa utetezi, uliwakilishwa na Peter Kibatala, Jebra Kambole, Jeremiah Mtobesya na Dickson Matata.

Yafuatayo ni mahoijiana ya mawakili wa pande zote na Shahidi juuya ushahidi wake:-

Wakili Kweka: Unaishi wapi?

Shahidi: Manzese Tip Top.

Wakili Kweka: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Mfanyabiashara nauza mitumba, Manzese Bakhressa.

Wakili Kweka: Hapa eneo la Manzese upo tangu lini?

Shahidi: Sipo muda mrefu sana miaka miwili.

Wakili Kweka: Miaka miwili kwenye nini?

Shahidi: Shughuli ya biashara miaka miwili.

Wakili Kweka: Na kimaisha upo kwa muda gani?

Shahidi: Kwa  kuishi nipo siku nyingi?

Wakili Kweka: Hapa mahakamani ukiambiwa wewe ni Shabani Juma ni sahihi?

Shahidi: Sio sahihi.

Wakili Kweka: Kwanini?

Shahidi: Naitwa Shabani Hamisi.

Wakili Kweka: Unaweza kuithibitishia mahakama.

Shahidi: Ndio nina kitambulisho cha Taifa.

Wakili Kweka: Mnamo tarehe 29, Oktoba, 2018, ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa natokea nyumbani kwangu Manzese naelekea kwenye shughuli zangu Bakhressa na nilikuwa natoka asubuhi.

Wakili Kweka: Wakati gani?

Shahidi: Kati ya saa moja na saa mbili asubuhi.

Wakili Kweka: Ehee?

Shahidi: Nilipofika ofisini kwangu nikaona watu kikundi wanaongea.

Wakili Kweka: Baada ya kufika?

Shahidi: Ilibidi nisogee kusikiliza nini wanaongea.

Wakili Kweka: Baada kusikiliza?

Shahidi: Nilisikia watu wanaongea masuala ya polisi.

Wakili Kweka: Kwa maana ipi?

Shahidi: Polisi wameua watu.

Wakili Kweka: Wameua wapi?

Shahidi: Uvinza Kigoma.

Wakili Kweka: Unasema ulifika eneo lako la kazi ukawaona watu makundi kwa makundi uliuliza nini kinachoendelea?

Shahidi: Ndio.

Wakili Kweka: Ulimuuliza nani?

Shahidi: Rafiki yangu Abdillahi.

Wakili Kweka: Alikueleza nini?

Shahidi: Alinieleza kuwa jana Zitto alieleza kuwa polisi wameuwa watu huko Kigoma Uvinza na kibaya zaidi waliwafuata hospitali na kuwaua.

Wakili Kweka: Ulimuuliza Abdillahi ameitoa wapi?

Shahidi: Kwenye vyombo vya habari mbalimbali.

Wakili Kweka: Enhee?

Shahidi: Alinitolea simu yake kwenye Youtube kupitia Ayo TV na kweli nikamuona Zitto Kabwe akizungumzia masuala ya uchumi usalama wa raia na mali zao, Tundu Lissu, korosho na mengine yanayohusu usalama wa nchi.

Wakili Kweka: Katika ushahidi wako ulisema Bwana Abdillah alikueleza hayo uliyoyasema labda na wewe ulivyoangalia uliona iko?

Shahidi: Niliona tena alinistua zaidi pale Mheshimiwa Zitto alisema kuwa polisi wamewauwa watu kibaya zaidi waliwafuata eneo la tiba na kuwauwa.

Wakili Kweka: Hebu tueleze alikuwa nani mwengine hapo John, Paul Yusuph na wengineo?

Wakili Kweka: Umetueleza alikuwepo Mheshimiwa Zitto Kabwe unamjua?

Shahidi: Namuona kwenye TV na hata hapa Mahakamani nilipokuja kwenye hii kesi.

Wakili Kweka: Yupo hapa?

Shahidi: Ee yule pale kwenye kizimba.

Wakili Kweka: Ulisema umemuona kwenye mahakama ifanunulie mahakama ulimuona mahakamani ulikuja kufanya nini?

Shahidi: Nilikuja niliitwa kwenye kutoa ushahidi wa hii kesi, nilimuona hapo chini.

Shahidi: Mimi nilichukulia uzito kwa sababu haya mambo yapo kwa sababu Mheshimiwa Tundu Lissu alifanyiwa tukio kama hilo na hakuna chochote kilichotokea nikaona sasa hawa Polisi sio watu wazuri.

Wakili Kweka: Kazi ya polisi nini.

Shahidi: Kulinda raia na mali zao.

Wakili Kweka: Hebu mueleze hakimu kwamba uliona lile tukio uliliona kama ugaidi?

Shahidi: Ugaidi ni hatua ya kufanya mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia kama nilivyosikia mimi kwamba polisi waliwafanyia mauaji raia wasiokuwa na hatia.

Wakili Kweka: Baada ya hapo nini kilitokea?

Shahidi: Niliwachukia Jesho la Polisi hata walivyopita  na gari zao walizomewa wauaji  hao. Lakini pale tulipokaa kulikuwa na mtu mzima aliyeniita pembeni na kuniuliza juu ya hilo tukio na kuniomba namba ya simu.

Wakili Kweka: Ilikuwa saa ngapi?

Shahidi: Saa 3 asubuhi.

Wakili Kweka: Nini kilifuata.

Shahidi: Nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni RCO wa Kinondoni ilikuwa tarehe 30.

Shahidi: Nilienda polisi kesho yake tarehe 31 nikakutana na yule mzee na walinihoji baada ya hapo wakaniuliza upo tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani. “Nikamwambia nipo tayari kwa sababu hilo ni jambo la kijamii nilitoa maelezo”.

Wakili Kweka: Lini 

Shahidi: Terehe 31 

Wakili Kweka: Mwezi wa ngapi?

Shahidi: Sikumbuki ni kama mwezi wa nane wa nane hivi.

Wakili Kweka: Baada hapo?

Shahidi: Niliondoka na siku za mbele nilipigiwa simu na askari.

Wakili Kweka alimaliza kumuongoza Shahidi kutoa ushahidi wake na kumpa nafasi Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala aendelee na mahojiano na shahidi mahakamani hapo kama ifuatavyo:-

Kibatala: Ulikitoa kitambulisho na kuombwa ukitoe.

Shahidi: Sijaombwa.

Kibatala: Umeongozwa kusema nyumba unayoishi.

Shahidi: Sijaulizwa wangeniuliza ningeongea.

Kibatala: Unasema wewe kwamba ni mfanyabiashara wa nguo.

Kibatala: Uliongozwa kusema lolote kuhusu duka lako.

Shahidi: Sisi hatuna duka.

Kibatala: Uliongozwa.

Shahidi: Sijaulizwa.

Kibatala: Siku hizi kuna vitambulisho vya machinga na wewe ni mfanyabiashara hizo ulikumbuka kukitoa mahakamani kitambulisho chako?

Shahidi: Sijakitoa kwa sababu sijaambiwa nije nacho ningekuja nacho.

Kibatala: Uliongozwa kusema jerani yako pale kushoto au kulia ni nani pale unapofanya biashara zako labda tujue kweli wewe ni mfanyabiashara?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Tukumbushe mwezi na tarehe?

Shahidi: Tarehe 29, Oktoba.

Kibatala: Na leo hii ni tarehe ngapi?

Shahidi: Ni tareje 16 mwezi wa tano 2019.

Kibatala: Huyu  rafiki yako Abdillahi uliongozwa kutaja majina yake  mawili?

Shahidi: Anaitwa Abdillah Salum.

Kibatala: Uliongozwa kuyataja?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Uliongozwa kutaja aina ya simu ya Abdillah mlioitumia kuangalia YouTube?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Aliyeingia kwenye simu ni wewe au Abdillah?

Shahidi: Abdillah.

Kibatala: Hukuongozwa kusema chochote kama simu Abdillah ilichukuliwa na polisi?

Shahidi: Sijasema.

Kibatala: Uliongozwa kulinganisha ulichooneshwa na Abdillah kulinganisha ulichokiona mahali pengine?

Shahidi: Sina simu kubwa hizi smartphone.

Kibatala: Swali langu lipo pale. Uliongozwa kulinganisha ulichooneshwa na Abdillah kulinganisha ulichokiona mahali pengine?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Uliongozwa kusema kwamba wewe hujui kutumia Smartphone?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Wewe ndiye ambaye uliyeona ile video kwenye simu ya Abdillah uliongozwa kumwambia hakimu kuwa hii hapa video niliyoiona?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Ni sahihi kwamba leo ulipigiwa simu uje mahamakamni kuja kutoa ushahidi?

Shahidi: Hajanipigia simu.

Kibatala: Nini kilichokufanya uje leo mahakamani?

Shahidi: Nilipigiwa simu siku za nyuma nije hapa.

Kibatala: Ulipigiwa simu nani?

Shahidi: Wakili wa Serikali.

Kibatala: Uliongozwa kumshika bega Zitto Kabwe?

Shahidi: Sikuongozwa nimemuonesha.

Kibatala: Uliongozwa kutaja majina ya John na Paul ni sahihi?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Uliongozwa kutaja majina yao ya pili?

Shahidi: Sijaongozwa

Kibatala: Shahidi ni sahihi kwamba ulisema hata magari ya polisi yalizomewa kuwa wauaji?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Uliongozwa kusema kuwa hawa watu waliokuwa wanazomea walikamatwa?

Shahidi: Hawajakamatwa.

Kibatala: Uliongozwa.

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Ni sahihi kwamba hujataja namba yako ya simu.

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Naomba umwambie hakimu kama uliongozwa kutaja jina la askari aliyechukua majina yao?

Shahidi: Sijaongozwa.

Kibatala: Unafahamu kuwa Ayo TV walikuwa wana matatizo ya kisheria kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)?

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Uliongozwa kutaja vyombo mbalimbali ulivyoambiwa na Abdillah?

Shahidi: Sijavitaja.

Kibatala: Ulikwenda na nani Osterbay polisi?

Shahidi: Nilienda pekee yangu.

Kibatala: Ulienda kabla au baada ya tukio?

Shahidi: Nilienda baada ya tukio.

Kibatala: Hukumpa taarifa mtu yoyote kwamba umeitwa polisi?

Shahidi: Nilimpa taarifa mama yangu mzazi.

Kibatala: Ni sahihi ulivyokutana na RCO hukuwa na wasiwasi wowote ule?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Unatambua kuwa RCO ni Ofisa wa polisi?

Itaendelea …

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!