Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi kesi ya Zitto: Aeleza alivyoshuhudia maiti kijiji cha Mpeta
Habari za Siasa

Shahidi kesi ya Zitto: Aeleza alivyoshuhudia maiti kijiji cha Mpeta

Spread the love

GERALD Serikali shahidi wa sita kwenye kesi ya uchochezo inayomkabili Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameieleza mahakama kuwa alishuhudia miili ya watu kati ya 18 au 20 vichakani alipokuwa kwenye harakati za kurejesha amani kwenye kijiji cha Mpeta mkoani Kigoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Gerald amedai kuwa siku ya tarehe 19 Oktoba 2018, alipokelewa na wananchi na kuanza utaratibu wa kuzisaka silaha hizo aina ya SMG na Bastola ndipo alipokutana na miili ya watu waliofariki kwenye mapigano kwenye vichaka pamoja na kuripoti vifo hivyo lakini watu wa usalama walimsisitiza afanye kazi aliyoagizwa.

Ameeleza kuwa akiwa kijijini alishiriki mazishi ya watu wanne waliofariki kwenye mapigano ambao ni Salu Deus, Gisena Pembesi, Adam, na Mwananingo, pia alishuhudia miili ya watoto wawili waliokuwa wameungua moto ambao aliambiwa na wananchi kuwa askari walichoma moto nyumba na kupelekea vifo hivyo.

Amedai kuwa alifanikisha kurejesha amani Mpeta na kufanikiwa kupata silaha za jeshi la Polisi zilizopotea kwenye mapigano kwa njia ya diplomasia  mwezi Aprili 2019  na kupelekea taarifa kwa watu wa usalama.

Ameeleza hali ilikuwa shwari na alifanikiwa kurejesha maelewano kati ya Polisi na wananchi ingawa mpaka sasa wananchi hawana ushirikiano na Mkuu wa wilaya ya Uvinza.

Baada ya kufanikisha zoezi hilo ameieleza mahakama kuwa alitarajia Serikali ingemlipa fedha alizoahidiwa kwa kazi ya kujitoa muhanga aliyoifanya baadala yake hakulipwa mpaka kufikia leo.

“Pamoja na kujitoa muhanga kwa kufanya kazi hiyo serikali haijanilipa pesa zangu zaidi ya kunipuuza na kuniona sina thamani,” amedai Gerald.

Alipoulizwa kwanini amepewa kazi hiyo ameeleza kuwa alikuwa amepewa dhamana ya uamifu na wananchi wa eneo hilo kutokana na kutokuwa na hiyana kwenye pesa alizokuwa akipewa na wananchi mbalimbali alipokuwa akifanya nao biashara.

Ameeleza kuwa taarifa za uaminifu hizo zilitolewa na Ofisa Tarafa wa Nguruka, Thomas Sangai kwa maofisa wa usalama wa mkoa  baada ya kutafuta suluhu ya amani kwenye kijiji hicho ndipo alipoombwa kutoa msaada wa kuzungumza na wananchi juu ya amani kisha kuzitafuta bunduki mbili za polisi zilizopotea kwenye mapigano kwa ahadi ya kulipwa Sh 15 milioni.

Awali ameeleza kuwa alipofika kwenye kijiji cha Mpeta wananchi walimsikiliza kwa uaminifu wake na kwamba amewaeleza kuwa anawasalimu Rais  “anasema muwe na amani nchi ni yenu na masuala yote atayasimamia kama munavyomjua  kuwa ni muaminifu”

Amedai kuwa wananchi walishangilia salamu zile za rais na ziliwatoa kwenye sura ya hasira na kuwa na furaha.

Hata hivyo amezisoma mahakama barua alizoziandika kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kueleza lalamiko lake juu kuahidiwa pesa na Kaimu Mkuu wa Mkoa bila kulipwa, pia ameendika barua kwa Mkuu wa wilaya ya Uvinza kwa Naibu waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega.

Aliisoma barua ya tarehe 15 Julai 2019 iliyotoka kwa mkuu wa Wilaya ya Uvinza yenye saini ya Mwanamvua Mrindoka aliyoiandika tarehe 1 Januari 2020 aliyojibiwa kuwa barua yake inafanyiwa kazi.

Shauri hilo litaendeele Kesho saa 3 asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!