August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shahidi Jamhuri, Wakili wa Zitto neno kwa neno

Spread the love

SHAHIDI wa 13 kwenye kesi namba 237/2018, inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Philbert Katundu, amesema hakuona tatizo kwenye mkutano wa kiongozi huyo na wanahabari. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Katundu ambaye ndiye mpelelezi wa shauri hilo, alitoa kauli hiyo tarehe 22 Oktoba 2019, mbele ya Hakimu Mfawidhi Huruma wakati akitoa ushahidi wake.

Awali, shahidi huyo aliyeongozwa na Wakili wa Serikali, Nassor Katuga aliieleza mahakama hiyo, kwamba yeye ndiye aliyeongoza jopo la makachero kwenye kupeleleza shauri hilo pia ndiye alimhoji mtuhumiwa huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=E_5y-HY9BfY

Baada ya kuongozwa shahidi huyo, alihojiwa na mawakili wa utetezi waliongozwa na Peter Kibatala, Frank Mwakibolwa, Jebra Kambole na Bonifasia Mapunda. Mahojiano hayo kama yafuatayo:-

Kibatala: Shahidi umekuwa polisi kwa kipindi gani?

Shahidi: Miaka 23.

Kibatala:Nitakuwa sahihi kuwa una uzoefu kwenye kazi hiyo?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni kifungu gani cha sheria kinawataka viongozi wa kisiasa, kupata kibali cha kufanya press-conference (mkutano na wanahabari)

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Watakaofanya Press-release uliyoisema polisi wote munaita Press-release ni Press Conference, wawe na Kibali ni kwa chama cha siasa tu au hata kwa taasisi yoyote?

Shahidi: Wote wanastahili kupewa kibali.

Kibatala: Klabu ya Simba wakitaka kufanya Press-Conference, ni lazima wawe na kibali?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Ni sahihi baada ya polisi kwenda kwenye tukio la press ya Zitto, walikupa taarifa yoyote ya kipelelezi?

Shahidi: Sahihi

Hakimu aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 22 Novemba 2019.

error: Content is protected !!