Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi amsukumia ‘zigo’ Mbowe, wenzake
Habari za Siasa

Shahidi amsukumia ‘zigo’ Mbowe, wenzake

Spread the love

SHAHIDI namba 7 katika kesi Namba 112 ya mwaka 2018, inayowakabili viongozi wa Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amedai kwamba ni kosa mawakala wa uchaguzi kufuata barua za utambulisho katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Shahidi huyo Victoria Wihenge ambaye ni Ofisa wa Uchaguzi katika Manispaa ya Kinondoni, amedai hayo leo tarehe 29 Agosti 2019, wakati akihojiwa na wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Mbowe, viongozi wengine wa Chadema na wafuasi wao, tarehe 16 Februari 2018 walidaiwa kufanya maandamano ya kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuchukua barua za utambulisho wa mawakala wao kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo ka Kinondoni uliofanyika tarehe 17 Februari 2018.

Kesi hiyo Mbowe ambaye ni Mwenyekiyi wa Chadema Taifa yupo pamoja na viongozi wenzake wa chama hicho ambao ni Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu –Zanzibar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Katika mahojiano hayo leo, shahidi huyo ameileza mahakama kwamba ni kosa mawakala kwenda kuulizia barua ambazo hazitolewi kwao, bali zinapelekwa katika vituo vyao vya kupigia kura.

Wakili; Wakitokea mawakala 10 wameenda kwenye vituo hawajakuta barua zao, wakaamua kuja kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kufuata barua, wanakuwa wamefanya kosa?

Shahidi; Ndio mheshimiwa

Wakili; Ni kosa gani wanakua wamefanya?

Shahidi; Kwenda kuulizia barua ambayo haijaandikwa kwao bali imeandikwa kupelekwa kwenye vituo.

Wakili; Watu watatu walienda kuuliza hati za viapo ofisini kwako, hao wamefanyakosa?

Shahidi; Hawakuja kwa maandamano hivyo hawakufanya kosa.

Wakili; Kuna watu waliokuja kwa maandamano ofisini kwako kudai barua?

Shahidi; Hakuna mtu aliyekuja.

Wakili; Ni sahihi wakala kuondoka na nakala za kiapo?

Shahidi; Sio sahihi wakala kuondoka na nakala za kiapo.

Wakili; Ni sahihi kabla ya tarehe ya uchaguzi, taratibu zote ziwe zimekamilika. Ni sahihi sio sahihi?

Shahidi; Sio sahihi.

Licha ya kudai kwamba ni kosa mawakala kufuata barua za utambulisho kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo, shahidi huyo ameeleza kwamba hawajapokea malalamiko kutoka kwa chama chochote kuhusu mawakala kunyimwa barua.

Wakili; Ni sahihi kwamba barua zilifika katika vituo vya kupiga kura?

Shahidi; Ndio mheshimiwa.

Wakili; Na ni sahihi wakala akipewa barua za utambulisho anatakiwa asaini?

Shahidi; Sio sahihi mheshimiwa

Wakili; Kwa hiyo alikuwa anaoneshwa barua ili akasimamie upigaji kura?

Shahidi; Hapana mheshimiwa, kwamba wakala anaonesha barua ndio akubaliwe kusimamia uchaguzi, bali wakala alitakiwa ajitambulishe kwa msimamizi na msimamizi anangalia barua ndio anamruhusu aingie.

Wakili; Wasaidizi wa chini walipokea barua?

Shahidi; Wasaidizi wote wa vituo walipatiwa barua hizo sambamba na vifaa vya uchaguzi.

Wakili; Mlitoa nyaraka zinazothibitisha barua zimetolewa kwa wasimamizi?

Shahidi; Hapana

Wakili; Ni sahihi tarehe 17 Februari 2018, wewe ulikuwepo ofisini wakati zoezi la upigaji kura linaendelea?

Shahidi; Nilikuwepo katika ofisi yangu au eneo langu la kazi.

Wakili; Ni sahihi ulikua hujui kama kuna malalamiko kwamba mawakala wamenyimwa barua kwa kila kituo?

Shahidi; Hakuna lalamiko nililopokea mheshimiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!