Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi amkwamisha Zitto Kisutu
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi amkwamisha Zitto Kisutu

Spread the love

KESI ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma mjini, imekwama kuendelea kusikilizwa leo katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Tumaini Kweka, Wakili wa Serikali amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kuwa, shahidi aliyetarjiwa kutoa ushahidi leo tarehe 9 Aprili 2019, amepangiwa majukumu mengine ya kikazi.

Ni mara ya nne sasa kesi hiyo inaahirishwa. Tarehe 29 Januari na 27 Februari shahidi alipatwa dharura.

Pia terehe 11 Machi, Zitto hakufika mahakamani akidaiwa kuumwa.

Ingawa Zitto amefika mahakamani lakini kesi yake imeahirishwa baada ya shahidi wa serikali kushindwa hakufika.

Hakimu Shahidi ameahirisha kesi mpaka tarehe 24 na 25 Aprili mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi hiyo.

Zitto alifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza, tarehe 2 Novemba 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018.

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Katika shitaka la kwanza, inadaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi.

Alitoa maneno ya uchochezi kuwa watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua.

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo ni ya uchochezi yenye kuleta hisia za hofu na chuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!