Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi akwamisha tena kesi ya Zitto Kabwe
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi akwamisha tena kesi ya Zitto Kabwe

Zitto Kabwe
Spread the love

SHAHIDI wa Serikali katika kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo amekwamisha tena kesi hiyo kwa kinachodaiwa kuwa amepata dharura iliyomfanya ashindwe katika ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa ushahidi wake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hii ni mara ya pili kwa kesi hiyo kuhairishwa kwani awali tarehe 29 Januari, mwaka huu kesi hiyo ilikwama kusikilizwa kwa madai kuwa shahidi alipata na matatizo ya kifamilia.

Mbele ya Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi Mkuu kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo tarehe 27 Februari mwaka 2019 ambapo Wankyo Simon, Wakili wa Serikali, amedai shahidi amepata dharura.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 11 Machi 2019.

Zitto alifikishwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza, tarehe 2 Novemba 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018.

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Katika shitaka la kwanza, inadaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi.

Alitoa maneno ya uchochezi kuwa watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua.

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo ni ya uchochezi yenye kuleta hisia za hofu na chuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!