Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi akwamisha kesi ya Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi akwamisha kesi ya Mbowe

Spread the love

 

KESI ya uhujumi uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, imeahirishwa hadi Jumatano, tarehe 26 Januari 2022, kutokana na shahidi wa Jamhuri kupata udhuru. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar ea Salaam … (endelea).

Kesi hiyo inayosikilizwa mfululizo imeahirishwa na Jaji Joachim Tiganga, baada ya Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, kuomba ahirisho akidai shahidi waliyekuwa wanamtegemea amepata dharura na kushindwa kutoka mkoani kuja Dar es Salaam, ilipo mahakama hiyo.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo yenye mashtaka ya ugaidi, ni waliokuwa makomandoo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Jaji Tiganga aliuamuru upande wa mashtaka umlete shahidi siku hiyo, ili kesi hiyo iendelee kusikilizwa.

“Nimesikia hoja iliyoletwa na upande wa mashtaka kuhusu ahirisho na sababu ambazo zimetolewa na mahakama kwa kuzingatia ukweli kwamba shauri hili tulipanga kuendesha mfululizo, naelekeza tarehe 26 Januari 2022, shahidi awepo ili tuendele kusikiliza shauri hili. Jitahidini kuleta shahidi kama ambavyo mahakama imeleekeza,” amesema Jaji Tiganga.

Awali, Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Wakili Peter Kibatala, aliuomba upande wa mashtaka watimize wajibu wao wa kuleta shahidi ili wateja wao wafahamu hatma yao mapema.

“Tunawakumbusha tu wenzetu kuwa, washtakiwa wanasubiria kwa hamu kufahamu hatma yao na wenzetu wafikire kama ingekuwa ndugu zao wako huko au wao wenyewe wangefanyaje? Ni hayo tu, mengine tunaiachia mahakama,” amedai Kibatala.

Wakili Kidando aliomba ahirisho hilo baada ya shahidi wa 11 wa Jamhuri, Askari Mpelelezi, Goodluck Minja, kumaliza kutoa ushahidi wake, alioanza kuutoa Ijumaa iliyopita.

Katika ushahidi wake, Minja aliieleza mahakama hiyo namna aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha, ACP Ramadhan Kingai, alivyounda kikosi kazi cha kudhibiti kikundi kinachodaiwa kuratibiwa na Mbowe, kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

Mbowe na wenzake wanadaiwa kupanga njama za vitendo vya ugaidi, ikiwemo kudhuru viongozi wa Serikali, kupanga maandamano yasiyo na kikomo, kulipua vituo vya mafuta na mikusanyiko ya watu, katika maeneo mbalimbali nchini.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai na Agosti 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!