Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi akwamisha kesi ya Halima Mdee
Habari za Siasa

Shahidi akwamisha kesi ya Halima Mdee

Ester Bulaya na Halima Mdee walipowasili kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam
Spread the love

KESI inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu,  ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli imekwama kusikilizwa leo tarehe 8 Oktoba 2018 baada ya shahidi upande wa mashtaka kushindwa kufika mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Katika kesi hiyo, mashahidi upande wa mashtaka walitakiwa kutoa ushahidi wao, lakini hawakufika kitendo kilichosababisha upande wa mashataka kukosa shahidi na kesi hiyo kuahirishwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipanga tarehe 22 Oktoba  2018 kesi hiyo kuendelea kusikilizwa baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita kudai kwamba shahidi waliyemtarajia kufika mahakamani hapo leo, yuko nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Licha ya kuiahirisha kesi hiyo, Hakimu Simba amesema kesi hiyo ifikapo mwezi Desemba mwaka huu iwe imeisha.

Mashahidi watatu akiwemo Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki upande wa mashtaka tayari wameshatoa ushahidi kuhusu kesi hiyo.

Mdee anadaiwa mnamo tarehe 3 Julai 2017 akiwa katika makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam alitoa lugha chafu dhidi ya rais Magufuli.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa  afungwe breki.”

Kauli hiyo inadaiwa kwamba ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!