Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi adai kushtushwa wenzake Mbowe kutuhumiwa kwa ugaidi
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi adai kushtushwa wenzake Mbowe kutuhumiwa kwa ugaidi

Spread the love

 

SHAHIDI namba tatu wa Jamhuri, katika shauri dogo la kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, Askari Polisi H4323 Msemwa, amedai alishtuka baada ya kusikia watuhumiwa wawili aliokabidhiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa hao ni, Adam Kasekwa na Mohammed Abdallah Ling’wenya, ambao ni washtakiwa wenza na Mbowe, katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanua vitendo vya kigaidi.

Msemwa ametoa madai hayo leo Jumatatu, tarehe 20 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar ea Salaam, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Msemwa ametoa madai hayo alipoulizwa na Wakili Katuga aliwatambuaje watuhumiwa wawili aliokabidhiwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Arusha, ACP Ramadhan Kingai awaweke katika mahabusu ya Kituo cha Polisi Kati cha Dar es Salaam.

Shahidi huyo wa jamhuri amedai, aliwatambua watuhumiwa hao, kutokana na upekee wa uhusika wao na kudai tangu alipokaa kituoni hapo kwa miaka sita (2014-2020), hajawahi kusikia gaidi.

Hivyo, alivyosikia kosa la watuhumiwa ni la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi alishtuka kidogo kisha akawaangalia.

Akitoa ushahidi wake, Msemwa amedai aliwapokea watuhumiwa hao wakiwa na hali nzuri kiafya, pia hata watuhumiwa hao waliporudi baada ya kuhojiwa alipowauliza afya zao walisema wako vizuri.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake katika shauri hilo, ambapo upande wa jamhuri umepanga kuita mashahidi saba.

Kwa sasa anahojiwa na mawakili wa utetezi, baada ya kuhojiwa na mawakili wa jamhuri.

Shauri hilo lilitokana na mapinganizi ya Mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda Kingai, katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, katika mapingamizi hayo walihoji kwa nini mtuhumiwa alihojiwa Dar es Salaam, badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!