KUELEKEA mchezo wa Fainali wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation), Shabiki wa klabu ya Yanga, Iddi Mkuu (69) ametinga Kigoma leo akitokea Arusha kwa kutumia baiskeli kushuhudia mchezo huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma … (endelea).
Mchezo huo ambao utawakutanisha mafahari wawili Simba dhidi ya Yanga, utapigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma tarehe 25 Julai, 2021 kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Shabiki huyo ambaye ametumia siku kumi njiani, huku akiendesha baiskeli kwa kilomita Zaidi ya 1,000.
Baada ya kuwasili Kigoma, shabiki huyo wa Yanga alipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa klabu hiyo na kumpeleka kwenye moja ya tawi lao.
Akizungumza na MwanaHALISI Online, shabiki huyo alisema, amekuja kushuhudia fainali hiyo licha ya kukutana na changamoto njiani.
“Nimekuja kushuhudia fainali ya FA hapa kigoma na wakati natoka kule nilipanga nifike hapa ndani ya siku 10.
“Changamoto zipo, kuna wanyama wakali mbugani na nilikutana na Twiga na akanipisha mimi nikaenda zangu,” alisema shabiki huyo.
Safari ya shabiki huyo kutoka mkoani Arusha ilianza jioni ya tarehe 12, siku ya Jumatatu na kufika mkoani Kigoma leo tarehe 21 Julai, 2021.
Leave a comment