May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shabiki Simba ajinyonga, siku ya mchezo dhidi ya Mbeya city

Spread the love

 

SHABIKI wa klabu ya Simba Khalfan Mwambena mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa kata ya Kholobe mkoani Mbeya amekutwa amejinyonga muda mchache kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Simba na Mbeya City. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kupitia taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu ya Simba hii leo, Tarehe 19 Januari 2021 ilieleza kuwa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Christina Musyani alithibitisha kuwa marehe alijinyonga kabla ya mchezo huo na si baada ya mchezo huo kama watu wengi wanavyoripoti.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipigwa kwenye dimba la sokoine tarehe 17 Januari, 2021 ambapo Simba alipoteza kwa bao 1-0, bao la dakika 19 lililofungwa na Paul Nonga.

Taarifa ya klabu ya Simba iliyomnukuu kamanda Musyani iliendelea kueleza kuwa, marehemu aliacha ujumbe kwenye karatasi uliosemeka kuwa “ Naipenda sana Simba na nikifa nizikwe na jezi ya Simba”

Licha ya kupoteza mchezo huo Simba imeendelea kusalia kwenye nafasi ya pili, wakiwa na pointi zao 24 pointi nane nyuma ya Yanga wenye alama 32 ambao wapo kwenye kilele cha msimamo huo.

Simba imepoteza mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, toka kuanza kwa msimu mpya wa 2021/22 mara baada ya kucheza dakika 919, sawa na michezo 11.

error: Content is protected !!