Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sh54 Bil. kugharamia mradi wa maji Chiuwe
Habari za Siasa

Sh54 Bil. kugharamia mradi wa maji Chiuwe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Chiuwe
Spread the love

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa Sh54 bilioni kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji wa Chiuwe utakaohudumia wilaya za Ruangwa na Nachingwea. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ameyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Julai 4, 2022) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi katika vijiji vya Mchenganyumba, Mbecha na Chimbila ‘B’ akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya Ruangwa.

Majaliwa amesema maeneo mengi ya wilaya hiyo maji yake ni ya chumvi, hivyo Serikali ilifanya utafiti na kubaini kuwa chanzo cha maji cha Chiuwe maji yake hayana chumvi na ni ya kutosha kuweza kuhudumia vijiji vya wilaya hiyo na wilaya jirani ya Nachingwea.

Ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kitakachowezesha kutekelezwa kwa mradi huo ambao kukamilika kwake kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika wilaya hiyo.

Baadhi ya wakazi wa Chiuwe

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kujiandaa kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa na viongozi kwenye maeneo wanayoishi. Zoezi hilo limepangwa kufanyika nchini kote Agosti 23, 2022.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wa wilaya ya Ruangwa Mhandisi Lawrence Mapunda amesema mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza itahusisha vijiji 34 vya wilaya ya Ruangwa na vijiji 21 vya wilaya ya Nachingwea.

Mhandisi Mapunda amesema ujenzi wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 utakamilika mwaka 2025/2026. “Kwa sasa utekelezaji wa mradi huu upo katika hatua ya manunuzi na unatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu kwa awamu zote.”

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la upatikanaji maji wilayani Ruangwa kwa zaidi ya asilimia 80. Chanzo cha maji cha Chiuwe kilichopo Nyangao kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 15 kwa siku huku mahitaji ya wilaya ya Ruangwa kwa siku ni tani milioni tisa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!