Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sh bilioni 1.3 kukamilisha mradi wa maji Dodoma
Habari za Siasa

Sh bilioni 1.3 kukamilisha mradi wa maji Dodoma

Juma Aweso, Waziri wa Maji
Spread the love

 

SERIKALI imetoa kiasi cha Sh. bilioni 1.3 kukamilisha mradi wa maji kwa wakazi wa Njendengwa, Ihumwa, Nzuguni, Nyumba miatatu, Iyumbu, soko kuu la Ndugai na FFU jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 30 Agosti, 2021 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipofanya ziara ya kwenye mradi huo wenye thamani ya Sh. bilioni 2.7.

Aweso amesema awali serikali ilitoa kiasi cha Sh. bilioni 1.4 kwa lengo la kuifanya makao makuu ya nchi kuondokana na adha ya maji ambayo ilikuwa ikiwakumba wananchi.

“Tunajua serikali inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hasan ni serikali ambayo inawajali wananchi wa hali ya chini.

“Pamoja na kuwajali watu wa hali ya chini inakusudia kumtua mama ndoo kichwani kwa maana hiyo mama yetu Samia ameona ni vyema kuwawezesha wakazi wa Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi, kiasi cha sh bilioni 2.7 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika maeneo tajwa.

“Awali Rais alitoa kiasi cha sh.bilioni 1.4 kwa ajili ya mradi huo wa maji,na sasa nimefanya ziara ya kutembelea na nimejiridhisha kuwa mradi unaenda vizuri, kwa maana hiyo sasa namuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Antony Sanga kuhakikisha anatoa fedha zilizobaki kwa ajili ya kumaliza mradi huo ili kutatua changamoto ya maji katika jiji la Dodoma ” amesema Aweso.

Jiji la Dodoma

Pamoja na kuagiza fedha hizo zitolewe pia amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira( DUWASA), Mhandisi Aron Joseph kuhakikisha anasimamia mradi huo na kukamilika ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.

Sambamba na hilo ameiangiza Bodi ya DUWASA kuona namna bora ya kumpatia ajira, mhandisi wa kujitolea James Ryoba ambaye amekuwa akifanya kazi ya kuunganisha mabomba ya maji ya mradi huo kwa kujitolea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo pamoja na kuwa umefikia hatua mzuri lakini changamoto ni kuwepo kwa miamba wakati wa uchimbani wa mitaro ya utandazaji wa mabomba.

“Lakini nataka kukuambia mheshimiwa Waziri mwanzoni mradi ulikuwa ni sh bilioni 2.4 lakini kutokana na muwepo kwa janga la Covid-19 vifaa vilipanda na kusababisha mradi kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 2.7″amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!