October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sh. 170,000 yamponza Hakimu, mzazi mwenzake kufikishwa kortini

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), itamfikisha mahakamani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kilimatinde, Manyoni, Bahati Ilikunda na mzazi mwenzake, Haji Bwegege wanaotuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 350,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida…(endelea).

Taarifa ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 amesema, ofisi yake ilipokea kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kuwa Bahati anaomba rushwa ya Sh. 350,000.

Amesema, ilia toe upendeleo kwa mtoa taarifa kwenye shauri la madai namba 03/2020, shauri ambalo lipo mbele yake.

Elinipenda amesema, tarehe 28 Juni 2020 wilayani Manyoni Mkoa wa Singida maeneo ya kituo cha mabasi yanaendayo Dodoma, ofisi hii ilimkatama Haji Juma Bwegege ambaye ni mzazi mwenzake na Baki baada ya kupokea rushwa ya Sh. 170,000 ikiwa ni sehemu ya Sh.350,000.

“Uchunguzi wa Takukuru Mkoa wa Singida umejiridhisha Haji Bwegege na Bahati Ilikunda wana mahusiano ya kifamilia (wana motto waliyezaa pamoja) jambo linaloashiria uwezekano wa Bahati kumtumia Haji katika kupokea rushwa anazoziomba,” amesema Elinipenda.

          Soma zaidi:-

Amesema, ofisi ya Takukuru inatoa shukuran za dhati kwa Idara ya Mahakama mkoani humo kwa jinsi wanavyoshirikiana kwenye mapambano dhidi ya rushwa kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama ya Mkoa.

error: Content is protected !!