November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sh. 17.89 Bil kujenga mradi wa maji Mwanza

Bomba la maji safi

Spread the love

JUMLA ya Sh. 17.89 bilioni zimetolewa na Serikali,  kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Butimba jijini Mwanza. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa programu ya uboreshaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika miji ya kanda ya ziwa.

Akizingumza jana wakati wa hafla fupi ya utiaji wa saini ya ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza, Mhandisi Antony Sanga, alisema kukamilika kwa mradi huo utawezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 400, 000.

Mhandisi Sanga alisema kuwa mradi huo unatatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia jana, ambapo mradi huo utakuwa umekamilika.

Alisema serikali imetoa kiasi hicho cha fedha baada chanzo cha zamani cha Kapriointi kuelemewa na watumiaji wa huduma hiyo na kulazimika kujenga chanzo kipya cha Butimba.

Mhandisi Sanga alisema ujenzi wa mradi huo, utaanza kwa ukalazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji kutoka chanzo kipya hadi tenki la Igoma kupitia eneo la Sahwa.

“Eneo la Sahwa lina kipenyo cha milimita 600 (inchi 24) na urefu wa kilomita 16.95 pia kazi nyingi ambazo zitafanyika ni pamoja na ujenzi wa tenki la chini la ardhi la kuhifadhi maji lenye ukubwa wa lita 2, 000, 000.

“Eneo hili la Sahwa pia ndilo litakuwa linasambaza maji katika maeneo ya Buhongwa, Usagara (Misungwi) na Kisesa (Magu) ili kutatua kero ya upatikanaji wa maji maeneo ya pembezoni,” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alisema ujenzi wa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) ya china na Mhandisi mshauri ni Egis Consultant kutoka ufarasa.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi aliwataka wakazi wa maeneo hayo na maeneo mengi ya jiji la Mwanza kuwa na utamaduni wa kutunza miradi ya maji ili kuendelea kuwanufaisha kwa kipindi kirefu.

Alisema miradi mingi imekuwa ikihujumiwa na baadhi ya wananchi wenye hatua ambayo amewahimiza zaidi kuhakikisha walinda miradi ya maendeleo inayotekeleza na Serikali.

Aidha amemtaka mkandarasi wa mradi huo, kampuni ya CCECC ya chini kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa muda uliokusudiwa.

Mmoja wa wakazi wa Butimba, John Laurent alisema ujenzi wa mradi huo utawasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji ambalo lilikuwa kero kubwa kwao na katika maeneo mengine ambako mradi huo utapita.

error: Content is protected !!