Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Sethi amalizana na DPP, kutoka leo
Habari MchanganyikoTangulizi

Sethi amalizana na DPP, kutoka leo

Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Harbinder Seth
Spread the love

 

MFANYABIASHARA Harbinder Sethi, anayesota rumande kwa takribani miaka minne, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, anatarajiwa kutoka baada ya kumalizana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 16 Juni 2021 na DPP Mwakitalu, akizungumza na MwanaHALISI Online, kwa simu, kuhusu mwenendo wa kesi hiyo, iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

DPP Mwakitalu amesema, Sethi huenda akatoka leo, kama atakamilisha taratibu walizokubaliana katika mazungumzo ya makubaliano kisheria (Plea Bagaining), ya kumaliza kesi hiyo, ambayo ilikuwa na washtakiwa wengine wawili, Mfanyabiashara James Rugemalira na Wakili Joseph Makandege.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka amesema, alifanya mazungumzo na Sethi, baada ya kupitia upya mwenendo wa kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na. 27/2017, iliyofunguliwa mahakamani hapo Juni 2017.

“Kesi ya Sethi tunai-review (pitia, ) lakini Sethi leo atatoka. Leo tunamalizana naye. Mfanyabiashara huyo tumemalizana naye kwa Plea Bargaining, kuna makosa amekiri ataadhibiwa halafu leo atatoka,” amesema DPP Mwakitalu.

Hata hivyo, DPP Mwakitalu hakuweka bayana makubaliano yake na Sethi, kuhusu kumaliza kesi hiyo, akisema kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatoa taarifa zaidi kama itafikia uamuzi wa kumuacha huru mfanyabiashara huyo.

Sethi na wenzake wawili, wanakabiliwa na mashtaka 12 katika kesi hiyo, ikiwemo utakatishaji fedha, kula njama na kujihusisha na mtandao wa uhalifu.

Mengine ni, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, pamoja na kusababisha hasara kwa Serikali, zaidi ya Dola za Marekani 22 milioni na Sh, 309.46 bilioni.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, kati ya tarehe 18 Oktoba 2011 na tarehe 19 Machi 2014, jijini Dar es Salaam.

Sethi na wenzake wanadaiwa kujipatia fedha kinyume cha sheria, katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa ajili ya utekelezaji wa mkataba wa ununuzi wa umeme na umiliki wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!