SERIKALI nchini imepiga marufuku biashara ya maji na vyakula visivyoandaliwa katika mazingira mazuri ili kupunguza kuenea kwa ugojwa wa kipindupindu uliojitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro. Anaandika Faki Sosi … (endelea).
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Dk. Seif Rashid alipozungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wananchi wachukue tahadhari ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.
Amepiga marufuku biashara za vyakula na maji ya kufunga maarufu kama kandoro katika mikusanyiko mikubwa ya watu hususan katika kampeni.
Dk. Rashidi amesema kuwa, mama ntiliye wanatakiwa kuandaa vyakula katika mazingira mazuri na kuzingatia kanuni za afya.
Amesema kuwa, ugonjwa huo umeenea katika manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Morogoro.
“Wananchi wanatakiwa kuandaa vyakula katika mazingira mazuri na yaliyo salama, husasani mama ntiliye pia kunawa kwa maji ya moto na sabun,i” amesema Dk. Rashidi.
Pia amesema kuwa, tangu kulipuka kwa ugonjwa huo 15 Agosti mkoani Dar es Saalam hadi 24 Agosti idadi ya wagonjwa ni 230 waliofariki 7, na Mkoa wa Morogoro walioathirika ni 15 na aliyekufa ni mtu mmoja tangu 17 Agosti hadi kufikia 24 Agosti mwaka huu.
More Stories
Gharama kipimo cha corona Z’bar yapaa
COVID-19: Waziri Gwajima ‘matamko yametosha’
COVID-19: Serikali yaja na mambo manane