July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali “yazibua masikio” Sheria ya Mtandao

Professa Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Spread the love

KELELE za wadau kupinga Sheria mpya ya Uharifu wa Mtandao (Cyber Crime) iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni, wakidai inazuia uhuru wa habari, hatimaye zimeizibua masikio Serikali. Anaandia Pendo Omary … (endelea).

Sheria hiyo imeibua mvutano mkali ndani na nje ya Bunge. Wadau wa mawasiliano wanasema “inahatarisha uhuru wa habari na kuipa nafasi serikali kuficha taarifa zake. Ina kasoro nyingi na hivyo itawatia hatiani watu wengi bila kujua.”

Kutokana na mjadala huo, Rais Jakaya Kikwete amekuwa katika shinikizo la kumombwa asiisaini sheria hiyo pamoja na ile ya Takwimu hadi hapo zitakaporudishwa bungeni na kufanyiwa marekebisho.

Hata hivyo, kelele za wadau hao, zilififishwa na taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, kwamba Rais Kikwete atazisaini sheria hizo na kwamba kama kuna marekebisho yatafanyika baadaye.

Kizingiti hicho hakikuzima harakati za wadau. Baadhi yao tayari wameonesha nia ya kupiga hodi mahakamani kusaka haki ya Watanzania wenzao. Lakini sasa serikali imezibua masikio.

Waziri wa Mawasilano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, amewataka wadau wenye maoni ya kuboresha sheria hiyo kujitokeza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa amesema “Sheria hii sasa imeshasainiwa na Rais baada ya kupitia hatua zote za kuiboresha”.

Kwamba, “Hatua ya mwisho ilikuwa ni ile ya marekebisho yaliyofanywa na Bunge ambapo baadhi ya vifungu vilivyolalamikiwa viliboreshwa.

“Wabunge, wabalozi, wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano, waandishi, wanabloggers na wananchi kwa ujumla kama kuna yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii alate maoni hayo hapa wizarani.”

Prof. Mbarawa ameongeza kuwa, katika kutumia sheria hiyo na kama ilivyo kwa sheria yeyote nyingine patakapoonekana kuna mapungufu, marekebisho yatafanyika.

“Serikali kupitia wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, tutayatafakari na kuyafanyia kazi. Haitosaidia sana kusema huko pembeni, jukwaa zuri la kuleta maoni ni kupitia kwa wizara yangu,”amesema.

Kwa mujibu wa waziri huyo, sheria hiyo haitakuwa ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama itaonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

error: Content is protected !!