July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaweka nguvu barabara ya Handeni – Kiteto -Singida

Mhandisi Leonard Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetenga Sh. 6 Bilioni kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha 2020/21. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Tarehe 5 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma na Mhandisi Leonard Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wakati akijibu swali la Mohamed Monni, Mbunge wa Chemba.

Monni ameuliza; je, ni lini serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami kwa kuwa ipo kwenye Ilani na pia ahadi ya Rais?

Akijibu swali hilo, Mhandisi Chamuriho amesema, barabara ya Handeni – Kiberashi – Kwamtoro – Singida ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 461. Kati ya urefu huo, kilometa 111 zipo Mkoa wa Manyara, kilometa 171 mkoa wa Dodoma na kilometa 47.1 mkoa wa Singida.

“Barabara hii ni kiunganisha muhimu cha Mikoa ya Singida, Manyara, Dodoma na Kanda ya Pwani hasa Bandari ya Tanga na Dar es salaam. Kukamilika kwa barabara hii, kutapunguza idadi ya magari yanayopita katika barabara kuu ya kati kuelekea Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa.

“Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii,” amesema.

Amesema, kwa sasa serikali ipo katika maandalizi ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hiyo na kwamba, katika mwaka wa fedha 20202/21, jumla ya Sh. 6 Bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi huo.

error: Content is protected !!