Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali yaweka mapingamizi kesi ya Diaspora kudai uraia pacha
HabariHabari Mchanganyiko

Serikali yaweka mapingamizi kesi ya Diaspora kudai uraia pacha

Spread the love

SERIKALI imeweka mapingamizi ya awali katika kesi ya kikatiba Na. 18/2022, iliyofunguliwa na watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora), kwenye Mahakama Kuu, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam, kupinga baadhi ya vifungu vya sheria vinavyozuia uraia pacha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu, tarehe 20 Februari 2023 na Wakili anayewawakilisha wana Diaspora hao, Peter Kibatala, wakati kesi hiyo ilipoahirishwa hadi tarehe 2 Mei mwaka huu, baada ya kiongozi wa Jopo la Majaji watatu wanaoisikiliza, Jaji Mustafa Kambona Ismail, kuwa na majukumu mengine ya kiofisi.

Akielezea mapingamizi hayo, Wakili Kibatala anadai upande wa Serikali wanaipinga kesi hiyo kwa madai kwamba hati ya viapo vya waleta maombi kuwa na mapungufu, pamoja na kupingana na masharti ya lazima ya Sheria ya Kupambania Haki za Kikatiba, kifungu cha 4.

“Wanasema ule wito wa mahakama haujasainiwa na wateja wetu na sisi wenyewe hatujaelewa wanamaanisha nini. Tarehe 2 Mei 2023 tutakuja kupata particular zake ili tujadili. Kwenye kesi za namna hii haziwezi kupita bila mapingamizi,” amedai Wakili Kibatala.

Kesi hiyo iliyofunguliwa 2022 na baadhi ya Watanzania waishio ughaibuni, inasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama kuu, ambapo mbali na Jaji Ismail, wengine ni Jaji Obadia Bwegoge na Jaji Hamidu Rajab Mwanga.

Watanzania hao, Shaban Fundi, Patrick Nhigula na Emmanuel C. Emmanuel, waishio nchini Marekani; Restituta Kalemera na Nkole Muya waishio Uingereza pamoja na Bashir Kassam aishiye Canada, wamefungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wana Diaspora hao wanapinga vifungu vya 7 (1) na (2) (C), (4) (a) na (6) vya Sheria ya Uraia ya Tanzania iliyofanyiwa marekebisho 2002 na kifungu cha 23 (1) (h) na (1) na cha 27 (2) (a) cha Sheria ya Uhamiaji, iliyofanyiwa marekebisho 2016, wakidai vinakwenda kinyume na katiba ya nchi.

Wanadai kwamba vifungu hivyo vinaelekeza kwamba raia yeyote wa Tanzania anayechukua uraia wa nchi nyingine, moja kwa moja anakuwa amepoteza uraia wa Tanzania, kitu wanachodai kwamba kinakiuka haki ya kikatiba ambayo hainyang’anyiki ya kuwa raia wa kuzaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!