Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaweka mapingamizi kesi kupinga tozo miamala simu
Habari Mchanganyiko

Serikali yaweka mapingamizi kesi kupinga tozo miamala simu

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeweka mapingamizi matatu katika kesi Na. 14/2021, iliyofunguliwa na Odero Charles Odero, kupinga makato ya tozo ya miamala ya fedha kupitia simu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne tarehe 24 Agosti 2021 na Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata, wakati mapingamizi hayo yalipokwenda kusikilizwa mahakamani hapo mbele ya Jaji John Mgeta.

Wakili Malata amesema, katika pingamizi la kwanza, hoja ya Serikali ni kwamba, maombi ya mfungua kesi sio halali.

“Hoja ya kwanza ni kwamba, maombi ambayo yeye anayaomba mahakama impe ruhusa ya kuweza kuleta shauri la Judiciary Review (mapitio ya mahakama), ili ahoji uhalali wa uwepo wa sheria na kanuni zake kwa njia ya Judiciary Review, tukasema si halali na tuna amini si halali kisheria,” amesema Wakili Malata.

Akifafanua pingamizi la pili, Wakili Malata amesema wanapinga kiapo cha mleta maombi kwa madai kwamba ni batili kwa kuwa taarifa zilizomo ndani yake sio za mleta maombi, bali alizitoa kwa mtu mwingine.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

“Kiapo ambacho kimeletwa na wakili ambaye ni John Seka, wakili wake na kiapo kimeletwa na Odero. Kinamtaja taarifa alizopata Odero alizitoa kutoka wakili wake, kisheria kama hizo taarifa ulizosema wewe muapaji zimetoka kwa mtu mwingine, huyo mtu anatakiwa aape hili kuondoa mapungufu ya kiapo,”

“Ambayo yanakifanya kiapo kisiwe halali, ushahidi wa njia ya kiapo hairuhusiwi kuwa hear say evidence, kiapo hicho kinakuwa batili, kiapo kinachounga mkono maombi ni batili,” amesema Wakili Malata.

Pingamizi la mwisho ni, Serikali inadai mleta maombi haoneshi namna alivyoathirika na tozo hiyo moja kwa moja.

“Kwa mujibu wa mashauri ya aina hii ni kwamba kabla mtu hujafungua kesi na ndani ya shauri unatakiwa ujiulize una interest gani. Wewe umekuwa affected moja kwa moja, kwenye kesi kwa maoni yetu mdai ameleta kiapo na madai yake hasemi ameathiriwa kivipi na hilo jambo,” amesema Wakili Malata.

Amesema “ikamfanya alete makahakani, anawajibika kuhakikisha anaieleza mahakama wazi wazi kwamba yeye amekwazwa na imemuathiri namna gani. Unapoleta kesi unawajibika kisheria kueleza unatahirika vipi, kitu ambacho hakufanya.”

Wakili Malata amesema maamuzi ya mapingamizi hayo yatatolewa na mahakama hiyo tarehe 8 Septemba 2021.

Katika kesi hiyo, Odero anaiomba Mahakama Kuu ifanye mapitio kanuni za Sheria ya Taifa ya Mfumo wa Malipo, Sura ya 437, zilizoanisha makato ya tozo hiyo kupitia miamala ya fedha katika simu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!