December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yazitoa kifungoni hospitali za Marie Stopes

Spread the love

SERIKALI imeruhusu hospitali na zahanati za Shirika la Marie Stopes kuendelea kutoa huduma baada ya kufungiwa wiki kadhaa zilizopita kutokana na kukiuka miongozo na maelekezo ya utoaji huduma za afya. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto kupitia tamko lake ililotoa leo tarehe 17 Oktoba 2018, imelitaka shirika hilo kuzingatia miongozo na maelekezo waliyopewa na serikali.

“Serikali itaendelea na wajibu wake wa kuzisimamia taasisi zote zinazotoa huduma ya afya nchini, lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa miiko na maadili ya kitaaluma pamoja na kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo iliyopo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hospitali na zahanati za Marie Stopes ziliagizwa kusitisha kutoa huduma baada ya ukaguzi wa serikali kubainisha kwamba zinakiuka miongozo,na kwamba shirika hilo lilifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha muda mfupi na kuruhusiwa kuendelea na utoaji huduma kwa kushirikiana na serikali.

error: Content is protected !!