Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yatumia mil 768 kumtunza Faru Fausta
Habari za Siasa

Serikali yatumia mil 768 kumtunza Faru Fausta

Faru
Spread the love

JUMLA ya 768 milioni zinatumika kila mwaka kwa ajili ya kumtunza Faru Fausta katika hifadhi ya ya Ngorongoro, bunge imefahamika, anaandika Dany Tibason.

Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) alibainisha gharama hizo ambazo serikali ilikiri kuzitumia kwa ajili ya kumtunza faru huyo kwa madai kuwa ni gharama za kawaida kulingana na thamani na umuhimu wa mnyama huyo.

“Hifadhi ya Ngorongoro inatumia gharama kubwa ikiwa ni pamoja na kumtunza na kumlisha chakula Faru Fausta kiasi cha Sh 64 milioni kwa mwezi, je serikali ina mpango gani kuhusu huyu Faru Fausta,” amehoji Gekul.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alikiri kuwa ni kweli mnyama huyo anatunzwa kwa gharama kubwa kwa sababu ni mzee, hivyo ananyemelewa na magonjwa mbalimbali.

Waziri alitaja sababu ya kufanya hivyo kutokana na ukweli kuwa wanyama wa aina hiyo ni wachache katika hifadhi, akasema utafiti unafanyika na kufanya ukweli wa gharama kuwa mdogo kulingana na thamani inayopatikana.

Gharama hizo zilisababisha Mbunge Frank Mwakajoka kuomba mwongozo wa spika akisema: “Majibu ya waziri anasema Faru Fausta yupo na anatunzwa kwa Sh 64 milioni kwa mwezi hii tafsiri yake anatunzwa kwa Sh 768 milioni kwa mwaka, anatoa sifa eti kwa sababu ni mzee sana, naomba mwongozo wako kuhusu hili kwa sababu mnyama huyu hawezi kuigiza faida yoyote.”

Akitoa mwongozo wake Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema suala hilo analiachia wizara na wakalifanyie kazi.

Awali katika swali lake la msingi Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya alitaka kujua serikali ina mpango gani endelevu wa kuhakikisha hadhi ya hifadhi hii inabaki kwenye ubora wake kwa ajili ya vizazi vya leo na vijavyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema ni kweli hifadhi ya Ngorongoro ni muhimu na ina hadhi ya kipekee inayotokana na uwingi na ubora wa vivutio vyake ambavyo vinatambulika kitaifa na kimataifa.

Amesema kutokana na sifa hizo Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kupitia orodha yake ya maeneo ya urithi wa dunia limelipatia eneo hilo hadhi yya kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!