Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yatoa tahadhari kuhusu Ebola
Afya

Serikali yatoa tahadhari kuhusu Ebola

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

SERIKALI imetoa tahadhari kwa umma kuhusu uwepo wa tishio la ugonjwa wa Ebola kufuatia ugonjwa huo kulipuka nchi ya jirani ya Uganda. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Ummy ametoa tahadhari hiyo kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu baina ya nchi ya Uganda na Tanzania kupitia mipaka rasmi na isiyo rasmi. Huku akisema kwamba  mikoa ya Kagera, Mwanza na Kigoma iko kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na mlipuko wa Ebola.

Kufuatia tishio hilo, Ummy ameiagiza mikoa na halmashauri zote nchini kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na wizara yake katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

“Hivyo ninaitaka Mikoa na Halmashauri zote nchini kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na @wizara_afyatz katika kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola. Aidha ninawataka wananchi ktk mikoa yote kuchukua hatua stahiki za kujikinga na ugonjwa huu ili usiingie nchini. #TishioLaEbola,” inaeleza taarifa ya Ummy.

Aidha, Ummy amefanya ziara katika Uwanja wa Ndege Mwanza na Kituo kipya cha kuwahudumia wagonjwa wa Ebola kilichopo Buswelu, Ilemela jijini Mwanza.

“Leo nimefanya ziara katika uwanja wa ndege Mwanza na Kituo kipya cha kuwahudumia wagonjwa wa Ebola kilichopo Buswelu, Ilemela jijini Mwanza. Lengo ni kupima utayari wetu wa kukabiliana na ugonjwa huu nchini,” amesema Ummy na kuongeza.

“Hata hivyo, kwa hali ilivyo na kutokana na ukweli kuwa ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine ni kwamba takribani nchi nzima iko katika hatari ya kupata mlipuko wa ugonjwa huu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika

Spread the loveKATIKA kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba nchini,...

Afya

Ummy Mwalimu:Umeme wa uhakika tija kwa uboreshaji huduma za afya

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na...

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

Afya

Kipindupindu chabisha hodi Dar, wagonjwa 10 waripotiwa

Spread the love  Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka jijini Dar es salaam ambapo...

error: Content is protected !!