Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali yatoa Sh. 573 mil. kukamilisha wa ujenzi sekondari ulioanzishwa na wanakijiji
Elimu

Serikali yatoa Sh. 573 mil. kukamilisha wa ujenzi sekondari ulioanzishwa na wanakijiji

Spread the love

 

SERIKALI kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga Sh. 573 milioni, kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Wanyere, wilayani Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, katika mkutano wake na wanakijiji cha Wanyere, uliofanyika jana Jumatano.

“Bajeti ya 2023/24, Serikali itatoa Sh. 573 milioni kupitia mradi wake wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari mpya katika Kijiji cha Wanyere. Hii itakuwa shule ya pili katika Kata ya Suguti,” amesema Prof. Muhongo.

Prof. Muhongo ameishukuru Serikali ya Rais Samia, kwa kuendelea kutoa fedha za kuboresha miundombinu ya elimu jimboni humo, huku akitaka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, kutoa fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo.

Amesema fedha hizo zilizopangwa kutolewa na Serikali, zitaunga mkono juhudi za wananchi walioanza kujenga shule hiyo kwa nguvu na fedha zao.

Prof. Muhongo amesema, hadi sasa amechangka mifuko 100 ya saruji, wakati wananchi wakichagia Sh. 2. 5 milioni, saruji mifuko 30, pamoja na nguvu kazi.

“Kwa sasa wanakijiji cha Wanyere wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 30 kwenda na kurudi kutoka masomoni kwenye sekondari ya kata. Baadhi yao wamepanga vyumba na wanajipikia karibu na eneo la shule, hivyo shule hii ikikamilika itasaidia kuondoa changamoto hizo,” amesema Prof. Muhongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

Elimu

Vipaji Green Acres vyawafurahisha wazazi

Spread the love WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Green Acres, wamewapagawisha wazazi...

ElimuHabari Mchanganyiko

Mtwara Girls waondokana na changamoto ya maji

Spread the love  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana mkoani Mtwara...

Elimu

Rc Singida atoa siku 7 kukamilisha miradi elimu ya sekondari

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Singida Peter Selukamba ametoa siku saba...

error: Content is protected !!