May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatoa ruzuku ya Bil. 100/- kushusha bei mafuta

January Makamba, Waziri wa Nishati

Spread the love

 

SERIKALI imetopa ruzuku ya Sh 100 bilioni kwa kipindi cha mwezi mmoja kwaajili ya kuleta ahueni katika bei ya nishati ya mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma … (endelea)

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 10 Mei, 2022 na Waziri wa Nishati, January Makamba wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya Serikali kuhusu hatua za dharura za kupunguza bei ya nishati ya mafuta.

Makamba amesema hatua hiyo inatokana na mahitaji ya wananchi, maoni na ushauri wa Wabunge, maelekezo ya Chama cha Mapinduzi.

Aidha amesema pia hatua hiyo imetokana na maelekezo ya Rais Samia kwamba ahueni ya bei ya mafuta itafutwe mapema badala ya kusubiri mwaka ujao wa fedha.

Hivyo basi, kama hatua ya dharura, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwamba, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha,

Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe Sh. 100 bilioni kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.

“Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2021/22.” Ameongeza Maakamba.
Amesema kutolewa kwa ruzuku hiyo hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea.

Mbali na ruzuku hiyo Makamba amesema nafuu nyingine itaanza mwaka ujao wa fedha kutokana na hatua ya Serikali kuomba mkopo kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

“Mchakato wa kuchukua mkopo huo uko mbioni kukamilika na ahueni kwenye kupanda kwa bei za bidhaa itapatikana katika mwaka ujao wa fedha,” amesema

error: Content is protected !!