SERIKALI ya Tanzania, imetoa muongozo na utaratibu wa wanafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali, kurudi shuleni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, akitoa taarifa ya mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, madarakani.
“Maagizo ya Rais ni kuhakikisha wote wanaweza kurudi na kumalizia masomo yao na hilo tayari wizara imeshatolea muongozo na utaratibu wa namna ya kurudi na natumia fursa hii tena kuwahimiza watoto walaiocha shule kuna fursa ya kurudi,” amesema Prof. Mkenda.
Waziri huyo wa elimu, amesema wanafunzi wanaotaka kurejea kwa mwalimu mkuu wa shule waliyokuwa wanasoma, ambapo kuna muongozo wa kamishna wa elimu unaoelezea utaratibu wa namna ya kurudi kwenye masomo.
Prof. Mkenda amesema, Rais Samia ana lengo la kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, ikiwemo wale waliokatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.
Leave a comment