November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatoa muongozo michezo Ligi Kuu

Uwanja wa Benjamin Mkapa

Spread the love

KUFUATIA kauli ya serikali kuruhusu shughuli za michezo kuendelea nchini iliyotolewa na Rais Magufuli, jijini Dodoma, 21 mei, 2020, Wizara ya Afya kushirikiana na Wizara ya Habari wametoa muongozo kwa wadau na mashabiki wa soka namna ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 kwenye viwanja vya michezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Katika muongo huo wa Serikali uliosainiwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Michezo, Harison Mwakyembe umeeleza kuwa wachezaji wakati wa mchezo hawatoruhusiwa kupeana mikono, kukumbatiana sambamba na kubadilishana jezi mara baada ya mchezo kukamilika kama ilivyokuwepo hapoa awali.

Wachezaji wote lazima kupimwa joto la mwili kabla ya mchezo huku vifaa vitakavyotumika kusafishwa kwa dawa na kuwekwa kwa mabango uwanjani na  kwenye vyumba vya kubadilishia nguo yenye kutoa maelekezo kwa mashabiki na wadau wa michezo kusoma kanuni na tahadhali za kuchukua dhidi ya maambukizi ya Covid 19.

Kwa upande wa mashabiki Serikali imeeleza kuwa lazima wamiliki wa viwanja lazima kuwepo kwa miundombinu ya upatikanaji wa maji tiririka na sabuni kwa ajiri ya kunawia mikono huku milango ya kuingia uwanjani kufunguliwa mapema na itumike kwa kuzingatia umbali wa mita moja.

Serikali imeeleza tena kuwa kama mashabiki wataruhusiwa watatakiwa kuzingatia umbali wa mita moja sambamba na wanahabari pamoja na wadau wengine watalazimika kuvaa barakoa wakati wote wa mchezo.

Aidha Serikali imeeleza kuwa wahusika na wamiliki wa viwanja lazima kuhakikisha kuwapo kwa gari la wagonjwa likiwa na vifaa muhimu ikiwemo vifaa vya kusaidia kupumua kwa ajiri ya tahadhari.

Tayari bodi ya Ligi jana kupitia kwa mtendaji wake mkuu Almasi Kasongo wametangaza rasmi kuwa michezo ya Ligi hiyo itarejea tena Juni 13, 2020 na ratiba kamili itapangwa Mei 31, 2020 ambapo michezo yote iliyosalia itachezwa kwenye kituo kimoja cha Dar es Salaam.

error: Content is protected !!