Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yatoa leseni mpya za madini
Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa leseni mpya za madini

Spread the love

LESENI mpya za madini takribani 7,879 zimetolewa na Tume ya Madini kuanzia mwezi Mei hadi Septemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika leo tarehe 4 Oktoba 2018 jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema leseni hizo zimetolewa baada ya maombi yake kupitishwa na kikao cha tume hiyo kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Akichanganua kuhusu leseni hizo, Prof. Kikula ameeleza kuwa, leseni za utafutaji wa madini zilizotolewa ni 263, leseni kubwa mpya zilizotolewa ni 3, leseni za uchimbaji wa kati 14 na leseni 1 ya sihia ya uchimbaji wa kati.

Prof. Kikula ameeleza kuwa, maombi ya leseni za uchimbaji wa kati 14 yaliyopitishwa yaliwasilishwa na kampuni za Dangote Industries Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya chokaa katika eneo la Mtwara; Nazareth Mining Investment Co Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) katika eneo la Ruangwa mkoani Lindi na kampuni ya Sunshine Mining (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini dhahabu katika eneo la Chunya mkoani Mbeya.

Aidha, Prof. Kikula amesema Tume imeweka mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwatengea maeneo maalum kwa ajili ya uchimbaji madini, ambapo amewataka kuunda vikundi na kusajiliwa kupitia viongozi wao hivyo kuwezesha upatikanaji wa leseni za madini na kufanya shughuli zao pasipo kikwazo chochote.

“Sisi kama Tume ya Madini tunatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na ndio maana tumekuwa tukifanya ziara katika maeneo ya wachimbaji wadogo na kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro; tunataka wafanye kazi katika mazingira salama kabisa,” alisema Profesa Kikula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!