Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yatoa ajira mpya za walimu
Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira mpya za walimu

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

SERIKALI imetoa ajira mpya za walimu 2,160 ambao wamepangwa katika shule za sekondari 1,721 nchini. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 20, Agosti, 2018, jijini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema, Kati ya walimu hao, walimu 1,900 ni wa masomo ya sayansi na hisabati.

Aidha alisema, walimu 100 ni wa masomo ya lugha na makundi sanifu wa maabara 160.

Jafo amesema,walimu hao wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za wakurugenzi wa Halmashauri zilizo shule walipopangiwa na baadaye kwenye shule.

“Walimu wote wanatakiwa kuripoti kuanzia Agosti 23 mwaka huu hadi Septemba 5 mwaka huu wakiwa na vyote halisi vya taaluma ya kidato cha nne na kidato cha Sita,cheti halisi vya kitaalam vya mafunzo ya ualimu vya ngazi husika na cheti halisi cha kuzaliwa,” alisema Jafo.

Amesema, waajiriwa wapya wote, vituo vyao vya kazi ni shule za sekondari walizopangiwa na siyo Makao Makuu ya Halmashauri huku akiwaonya kuacha tabia ya kuchukua posho ya kujikimu kisha asiripoti katika kituo chase cha kazi alichopangiwa.

“Katika hili naomba niwaeelekeze walimu wapya kulwa,Serikali haitasita kumchukulia hatma za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za Nchi,” alisisitiza.

Vile vile amesema, hakuna mwajiriwa atakayebadilishiwa kituo alichopangiwa kwa sababu yoyote ile, huku akiwatahadharisha walimu watakaochelewa kuripoti ndani ya muda uliotolewa kuwa,nafasi zao watapangiwa walimu wengine wenye Sita waliokuwa nafasi.

“Ikumbukwe kuwa, tulipotangaza maombi ya nafasi hizi,jumla ya walimu 20,101 walituma maombi yao,na waliopata ni hao 2,160,kwa hiyo atakayechelewa,Ofisi ya Rais Tamisemi, itatoa nafasi hiyo kwa mwombaji mwingine aliyekidhi vigezo,” amesema Jafo.

Jafo ametumia fursa hiyo kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu na fundi sanifu maabara hao wamepangwa ,kuwapokea kwa kuzingatia taratibu na kabuki zote za Utumishi na baadaye kutoa taarifa za kuripoti waajiriwa hao.

Amewaagiza kujaza taarifa hizo kwenye mfumo wa kielektroniki wa taarifa za watumishi wa ajira mpya katika Ofisi ya Rais Tamisemi mara baada ya kuripoti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

error: Content is protected !!