April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yathibitisha uwepo wa homa ya dengue Dar, Tanga

Spread the love

SERIKALI imetoa taarifa kwa Umma kuwa bado kuna ugonjwa wa homa wa Dengue hapa nchini licha ya kuwa ugonjwa huo, mpaka sasa hakuna kifo kilichotokana na ugonjwa huo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile alisema kuwa serikali inatoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya dengue hapa nchini na ugonjwa huo umeibuka tena na kuendelea kuthibitishwa nchini hususani katika majiji ya Dar es Salaam na Tanga kuanzia mwezi Januari 2019.

Alisema kwamba hadi kufikia terehe 2 Aprili 2019 kati ya watu 470 waliopimwa wagomjwa 307 wamethibitishwa kuwa na virusi au walishapata ugonjwa wa homa na kati yao hao 252 kutoka Dar es Saalam na 55 wanatoka Tanga.

“Katika jiji la Dar es Salaam wagonjwa wamethibiitishwa katika hospitali ya Mwananyamala, Ilala, Temeke, Vijibweni, Aga-Khani, Regency, IST na Ebrahim Haji.

“Kutoka katika jiji la Tanga wagonjwa wamethibitishwa katika hospitali za Bombo, Aga-Khan, Burhan Street 4 na Safi Medics,” alieleza Dk. Ndungulile.

Aidha alieleza kuwa ugonjwa huo siyo ugonjwa mpya nchini na katika miaka ya 2010, 2013,2014 na 2018 hasa ukizingatiwa uwepo wa mbu ambaye anaeneza ugonjwa huo.

Alieleza kuwa ugonjwa wa dengue unasababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aina ya “Aedes” ambao ni weusi wenye madoadoa meupe yenye kung’aa.

Alisema kuwa dalili za ugonjwa huo ni homa ya ghafla, kuumwa na kichwa hususani sehemu za mwili, maumivu ya viungo vya mwili na dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku tatu hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa na virusi ya dengue.

Alisema kuwa mgonjwa wa homa ya dengue hutibiwa kutokana na dalili zitakazo ambatana na ugonjwa huo kama vile homa, kupungukiwa damu au maji.

Kutokana na hali hiyo wizara inasisitiza wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu kama vile kufyeka majani, kuondoa madimbwi  kwa kuyafikia na kuondoa vifuu vya nazi au makopo yanayotuamisha maji.

Hata hivyo hivyo Dk. Ndungulie alitoa rai kwa watanzania wote ili waweze kujenga utamaduni wa kupima afya zao pale wanapojisikia kuwa na dalili tofauti badala ya kusubiri madhara makubwa yajitokeze.

error: Content is protected !!