Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Serikali yatenga Tril. 1/- kukopesha mabenki kwa riba ndogo
HabariTangulizi

Serikali yatenga Tril. 1/- kukopesha mabenki kwa riba ndogo

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Shilingi trilioni moja katika mpango mahususi wa kuwezesha mabenki kukopesha kwa riba ndogo isiyozidi asilimia 10. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rais Samia ameyasema hay oleo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa jengo la makao makuu ya benki ya CRDB.

“Serikali kupitia Benki Kuu imeanzisha mpango mahususi wa kuwezesha sekta za kibenki kupata mikopo yenye riba nafuu, ambapo Benki Kuu imetenga jumla ya Sh. Trilioni moja kwaajili ya kuwakopesha mabenki kwa masharti nafuu sana ikiwemo riba ndogo ya asilimia tatu,” amesema Rais Samia.

Amesema lengo la mpango huo ni kuongeza ukwasi wa mabenki na kuweza kukopesha sekta binafsi kwa riba ndogo isiyozidi asilimia 10.

Rais Samia ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuitikia wito wa Serikali kwa kweza kupunguza riba kufikia kiwango cha asilimia tisa na viwango vingine ambavyo wamepunguza kwenye makundi mbalimbali.

Aidha ametoa wito kwa mabenki kuhakikisha fedha watakazokopeshwa na Serikali kwa riba ndogo zisitumike kulipa madeni yao bali zielekezwe kukopesha sekta binafsi kama ilivyokusudiwa.

1 Comment

  • Kwanini serikali inapendelea benki za CRDB na NMB badala ya kuziachia zishindane na benki za binafsi? Kwa mfano malipo YOTE ya serikali na mashirika yake yanapitia CRDB na NNB.
    Kwanini serikali isiwaachie watumishi wake na wastaafu wake wachague benki wazipendazo badala ya kuwalazimisha watumie NMB na CRDB? Halafu tunaambiwa eti NMB na CRDB zinatengeneza faida zaidi na zinaongoza. Si kweli. Tuachane na Monopoly isiyosaidia wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!