Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yatenga Sh. 15 bilioni kukamilisha maboma 300 ya zahanati
Afya

Serikali yatenga Sh. 15 bilioni kukamilisha maboma 300 ya zahanati

Dk. Festo Dugange, Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Spread the love

 

SERIKALI imetenga kiasi cha fedha Sh. 15 bilioni, katika mwaka wa fedha wa 2022/23, kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa maboma ya zahanati 300. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Festo Dugange, bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 5 Aprili 2023, wakati akimjibu Mbunge wa Rorya Japhary Chege, aliyehoji lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati yaliyoanza kujengwa na wananchi.

Dugange amesema, hadi kufikia Februari 2023 fedha kiasi cha Sh. 14.6 bilioni, zimekwishatolewa.

Aidha, Dugange amesema kuanzia 2017/18 hadi 2021/22, Serikali imetumia kiasi cha Sh. 71.95 bilioni, zimetolewa kwa ajili ya ukamilishaji maboma ya zahanati 1,214 nchini kote.

“Jumla ya zahanati 762 kati ya 1,514 ujenzi umekamilika na zimeanza kutoa huduma. Aidha, ujenzi wa maboma 752 ya zahanati uko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ujenzi. Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa maboma yanayojengwa na wananchi,” amesema Dugange.

1 Comment

  • (xi) Mhe. WAZIRI Mkuu baada ya SERIKALI KUHAMIA DODOMA LINI VYOMBO VYA HABARI VYA ITV, EATV, TBC, AZAM TV, WASAFI TV, MWANANCHI VITAHAMIA DODOMA KWA LAZIMA.(TULIBUNI DSM HATUWEZI KUBUNI DODOMA)SWAHILI

    (xii) Dissertation (Confession Time):- Do high Unemployment Rate Influence Someone other Guys Creativity in solving PROBLEM, PRIDE, SOCIAL STATUS, WEALTH and Planning (TITANIC SOLVERS IN PARLIAMENT)?!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!