Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yatenga Bil. 30 kukarakabati hospitali za Rufaa
Afya

Serikali yatenga Bil. 30 kukarakabati hospitali za Rufaa

Spread the love

SERIKALI imetenga Sh. 30 bilioni kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya hospitali za Rufaa za Mikoa kila mkoa ili kuweza kuwawezesha wananchi kupata huduma za rufaa za kibingwa karibu na wanapoishi na hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati akiwasilisha taarifa za uendeshaji wa hospitali za rufaa za Mkoa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.

Dk. Ndugulile amesema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha hospitali za Rufaa za Mikoa ya Geita, Katavi, Simiyu, Njombe na Songwe ambapo zipo katika hatua za ujenzi wa hospitali hizo hivyo itafanya idadi ya hospitali hizo kuwa 28 pindi zitakapokamilika.

“Serikali ilifanya mabadiliko ya kuzihamishia hospitali za Rufaa za Mikoa Wizarani ili kuboresha huduma za kibingwa ikiwemo kutoa fursa nzuri ya udhibiti, usimamizi na mgawanyo wenye tija zaidi wa rasilimali chache zilizopo,” amesema Dk. Ndugulile.

Amesema kuwa baada ya wizara kukabidhiwa hospitali hizo ilifanya tathimini ya awali ya hali halisi na kubaini changamoto mbalimbali zilizoathiri utoaji wa huduma za afya katika maeneo yote ambayo ni nguzo ya msingi katika kuwezesha upatikanaji wa huduma bora.

“Hospitali za Rufaa za Mikoa zinapaswa kutoa huduma za kibingwa ambazo hazitolewi katika hospitali ngazi ya Halmashauri,Huduma za kibingwa ambazo ni lazima kupatikana katika hospitali za Rufaa,” amesema Dk. Ndugulile.

Amezitaja huduma za kibingwa ambazo zinatakiwa kutolewa katika hospitali hizo za Rufaa za Mikoa ni pamoja na upasuaji wa jumla,magonjwa ya uzazi na yanayoathiri wanawake, magonjwa ya watoto, magonjwa ya ndani, magonjwa ya kinywa na meno na Radilojia.

Kwa upande wa ubora wa huduma zinazotolewa Naibu Waziri huyo amesema Wizara ilifanya kaguzi za kuzitambua hali halisi ya ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na jumla ya hospitali za rufaa ishirini na moja zilifanyiwa tathimini na kupewa nyota kutokana na vigezo vilivyowekwa na kupewa mpango kazi wa kuboresha huduma.

“Ni hospitali tisa zilipata nyota mbili, hospitali kumi na moja zilipata nyota moja na hospitali moja ilipata nyota sifuri, hivyo hakuna hospitali yeyote iliyopata nyota 3 hapa nchini.” amesema Dk. Ndugulile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Dk. Biteko aagiza uboreshaji huduma za afya kwa wazee

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the loveWataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Madaktari wazawa watenganisha watoto mapacha walioungana

Spread the loveHospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara nyingine imeandika historia kwa...

Afya

DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu

Spread the loveMkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za...

error: Content is protected !!