September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatangaza uwezekano wa Ebola kusambaa kwa kasi

Spread the love

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonesha kuwa uwezekano wa kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola Tanzania umeongezeka maradufu. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea). 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara hiyo, Mwalimu amesema kuwa hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na Ebola katika nchi ya DR Congo ambapo hadi sasa

“Tumeona na sisi tuje kwa uzito huo huo ambao Shirika la Afya Duniani imeutoa tuweze kutoa tahadhari ya hali ya juu kwa watanzania,” amesema.

Ameeeleza kuwa hali hiyo ni uwezekano huo ni kutokana na eneo ambalo lililoathirika la Kivu Kaskazini lipo karibu na nchi jirani ya Uganda hivyo muingiliano wake wa watu baina ya DRC, Uganda na Rwanda na inapelekea uwezekano mkubwa Tanzania kupata maambukizi.

Hata hivyo Mwalimu amesema pamoja na tahadhari hiyo bado hakuna aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya iliyotolewa Agosti 10 mwaka huu wagonjwa 26 walikuwa wamefundulika kuwa na Ebola nchini DR Congo na vifo vilikuwa 10 lakini kwa taarifa ya leo Agosti 21 iliyotolewa na Wizara hiyo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani imeeleza kuwa idadi ya wagonjwa imeongezeka hadi kufikia 91 na vifo vilivyoripotiwa ni 50.

error: Content is protected !!