Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali yatangaza neema makato mikopo ya elimu ya juu
Habari

Serikali yatangaza neema makato mikopo ya elimu ya juu

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeahidi kufanyia mapitio kanuni za sheria ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu, ili kuondoa changamoto ya makato makubwa ya tozo na riba kwa wanufaika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 31 Machi 2021, na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Kipanga Omary, bungeni jijini Dodoma, baada ya mjadala wa mikopo ya elimu ya juu, kuibuliwa tena na wabunge, wakidai makato ni makubwa.

Kipanga amesema, katika mapitio hayo, Serikali itaangalia namna ya kupunguza ama kuondoa kabisa tozo na riba hizo.

“Ni kweli mnufaika anakatwa asimilia 15 ya tozo na makato haya yalipitishwa na Bunge, kuna asilimia 10 ya riba kwa watakaochelewa na asilimia sita.”

“Kama nilivyojibu mwanzo, tunakwenda kufanya mapitio ya kanuni hizi kuangalia aidha kuonda au kupunguza,” amesema Kipanga.

Kipanga Omary, Naibu Waziri wa Elimu

Majibu hayo ya Kipanga yametolewa kufuatia mjadala huo kuibuliwa na wabunge mbalimbali, waliohoji mpango wa Serikali kuwaondolea mzigo wa makato makubwa wanufaika wa mikopo hiyo.

Mbunge Viti Maalumu (asiye na chama bungeni), Halima Mdee, akiuliza swali alidai mikopo hiyo ni ya kibiashara kutokana na makato yake kuwa makubwa.

“Serikali imekuwa ikijinasibu kuwa mikopo inalenga kusaidia watoto wa familia masikini lakini kimsingi inakuwa mzigo kwa watoto wa masikini.”

“Asimilia 15 wanakatwa kila mwezi, asilimia 10 ya riba, asilimia sita kwa watu ambao hawana riba, badala ya kuwa ni mkopo wa kusaidia watoto unakuwa wa kibiashara,” amesema Mdee ambaye tarehe 27 Novemba 2020, alifukuzwa Chadema na wenzake 18 kwa usaliti.

Mdee amehoji “lini Serikali italeta bungeni mabadiliko ya kisheria ili kila kinachosemwa kinasaidia watoto wa masikini kinathibitishwa kwa maneno na vitendo, isiwe lugha za kisiasa.”

Naye Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole akiuliza swali, amehoji kwa nini Serikali isiwapunguzie kiasi cha riba, wanufaika wanaolipa madeni yao kwa mkupuo.

“Kwa nini Serikali isipunguze riba kwa hao wanaolipa deni lote kwa mkupuo au kwa wakati mmoja, kutoka asilimia 10 mpaka mbili au tatu?”

“Au na vilevile kupunguza tozo ambayo ni kubwa na haipo kwenye mkataba wanaojaza wakati wa kukopa,” amehoji Mwenisongole.

Baada ya mjadala huo kuibuka, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako naye alisimama kuhitimisha akisema, wanufaika wa mikopo hiyo wanaochelewa kulipa, hawatozwi asilimia 10 ya riba kama ilivyoelezwa na wabunge hao.

“Nampongeza waziri kwa majibu yake mazuri na maswali mengi ameyajibu kiufasaha, jambo dogo niweke kumbukumbu ili hata kwenye taarifa rasmi za bunge ikae vizuri.”

“Nilikuwa nataka kueleza katika mkopo mwanafunzi analipa asilimai sita kama tozo ya kutunza thamani, lakini na hakuna riba ya asilimia 10 kama ilivyoelezwa na hiyo asilimia sita ni ile ambayo tunaifanyia kazi, naomba kumbukumbu ikae vizuri,” amesema Prof. Ndalichako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!