Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yatangaza nafasi za kazi makarani, wasimamizi sensa
Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yatangaza nafasi za kazi makarani, wasimamizi sensa

Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene
Spread the love

SERIKALI imetangaza nafasi za kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa ya mwaka 2022 itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 5 Mei 2022 na Waziri wa Sheria na Katiba, George Simbachawene kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya mwaka 2022.

Simbachawene amesema watanzania wote wenye sifa zilizoanishwa wanaweza kuomba nafasi hizo kupitia mtandao kuanzia leo tarehe 5-19 Mei 2022.

“Ajira hizi zitaombwa kupitia mtandao na hazitahusisha malipo ya aina yeyote,” amesisitiza Simbachawene.

Ameeleza zaidi kuwa mchakato wa kuchambua maombi utafanyika katika kamati za sensa ngazi za wilaya na usahili utafanyika katika ngazi za kata kwa nafasi za makarani na wasimamizi.

Aliongeza kuwa wale wanaohusika na masuala ya TEHAMA usahili utafanyika katika ngazi ya Wilaya.

“Niwaombe watanzania wote wenye sifa ambao wangependa kuomba nafasi za kazi za makarani na wasimamizi wa sensa kufuata utaratibu uliowekwa kikamilifu ili kuomba nafasi hizi.” Amesisitiza.

Amesema kazi za kufanya pamoja na sifa za mwombaji zimebainishwa katika tangazo la ajira za muda za kazi za makarani na wasimamizi wa sensa ya mwaka 2022.

“Hakuna ombi litakalofanyiwa kazi ikiwa limeombwa nje ya uataratibu huu kwamba lazima aombe kwa njia ya mtandao.”
Ameongeza kuwa mfumo wa kuomba ajira hizo utapitia mtandao kwenye tovuti za www.pmo.go.tz; www.tamisemi.go.tz; www.nbs.go.tz kwa Tanzania bara na www.mpo.gr.tz kwa upande wa Zanzibar.

Amesema kupitia tovuti hizo waombaji watapata tangazo kamili la kazi lenye orodha za nafasi zilizopo katika sensa na orodha ya kazi za kufanya.

Aidha ameonya uwepo na baadhi ya makundi ambao wanatumia uwepo wa nafasi hizi za kazi kutapeli na kuharibu utaratibu mzima wa mchakato wa upatikanaji wa wafanyakazi wa sensa.

“Kwa kufanya hivyo si tu wanakiuka Sheria bali pia wanataka kuharibu zoezi zima la sensa kwahiyo matapeli hawa ambao wamekuwa wakitangaza matangazo hayo hayakuwa rasmi,” amesisitiza.

7 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!