December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatakiwa kuwakopesha wavuvi

Wavuvi wakiwa kazini

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuwakopesha zana za uvuvi vikundi vya wavuvi vilivyoko katika makambi yanayolizunguka Ziwa la Rukwa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo ulitolewa leo bungeni na Mbunge wa Kwela, (CCM) Ignas Malocha ambaye alitaka kujua ni lini serikali itavikopesha zana za uvuvi kama nyavu na injini za boti vikundi vya wavuvi walioko katika makambi yanayolizunguka Ziwa Rukwa.

Aidha, alihoji serikali ina mpango gani wa Kitaifa wa kulinusuru Ziwa Rukwa lisikauke kwani inasemekana kuwa liko hatarini kukauka baada ya miaka kadhaa.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Kaika Telele amesema serikali imeanza kuhakiki mfumo wa kutoa ruzuku kwa wavuvi wanaojiunga kwenye vyama vya ushirika vya wavuvi.

Amesema kiasi cha asilimia 40 ili wavuvi wachangie asilimia 60 katika bei ya zana za uvuvi zikiwemo boti, injini na viambana vyake.

Kuhusu kulinusuru ziwa Rukwa lisikauke, amesema kiasi cha maji katika mito na maziwa likiwemo ziwa Rukwa hubadilika kutegemeana na kiasi cha mvua inayonyesha katika bonde la ziwa hilo.

Amesema ziwa hilo hupata maji kutoka katika mito tisa ambayo ni ya Rungwa, Wuku, Chambua, Lukwate, Kikambo, Luika, Luicha, songwe na Kavuu.

error: Content is protected !!