
Wanafunzi wakisoma chini ya mti kutokana na kukosa madarasa
SERIKALI imetakiwa kutatua tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi za sekondari nchini badala ya kutegemea nguvu za wananchi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo na bungeni na Mbunge wa Mpanda mjini, Said Arfi (Chadema).
Arfi alitaka kujua serikali ina mpango gani wa muda mfupi na mrefu wa kutatua tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari nchini pamoja na madawati badala ya kutegemea nguvu za wananchi.
Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa alisema serikali imepanga kukarabati na kukamilisha shule za sekondari za wananchi 1,200 kwa kiwangl cha kuwa namiundombinu yote muhimu.
Amesema awamu ya kwanza imekamilisha shule 264 ambazo zilitengewa Sh. Bilioni 56.4 huku Sh. Bilioni 67.8 zitatolewa kwa ajili ya kuanza awamu ya pili kwa shule 528 na awamu ya tatu itakuwa na shule 408.
Aidha, amesema kati ya mwaka 2009 hadi 2014, serikali kupitia MMEM na MMES imetoa Sh. Bilioni 30.9 katika halmashauri zote nchini kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule.
Kuhusu madawati, amesema serikali kupitia mipango ya MMES na MMEM kati ya mwaka 2011 na 2013, imepeleka Sh. Bilioni 5.5 katika halmashauri zote kwa ajili ya madawati zikiwemo Sh. Milioni 358 zilizopelekwa Mpanda.
More Stories
Dirisha maombi mikopo elimu ya juu kufunguliwa Julai 15
Shule za Serikali, wasichana wang’ara matokeo kidato cha sita
Watakao kwamisha mradi wa kuboresha Elimu Sekondari kukiona