January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatakiwa kueleza athari za minara

Mnara wa simu ya kampuni ya Vidacom ukizinduliwa katika kijiji cha Lukanga wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Mariam Kisangi ameitaka serikali ieleze athari zitakazotokea kwa watu wanaoishi karibu na minara ya simu. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kisanga alitoa kauli hiyo leo  bungeni ambamo  amesema ujenzi wa minara ya simu katika makazi ya watu unaendelea katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali nchini.

“Je, minara hiyo ina athari gani kwa maisha ya watu waliokaribu na minata hiyo?”alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema  athari zinazoweza kusababishwa na mionzi ya radio ni ongezeko la joto mwilini pale mtu au mnyama anapokaribia chombo kinachorusha masafa kiitwacho antenna.

“Kwa vile nguvu iliyomo katika masafa inayosafirishwa na antenna zilizofungwa katika mnara wa mawasiliano hupungua kwa kiwango kikubwa sana kutoka mahali mnara ulipo, na kwa vile antenna hufungwa mita kadhaa juu ya minara, nguvu na mionzi hiyo huwa ni ndogo sana ifikapo chini ya minata ya kuweza kuleta athari yeyote,” amesema.

Amesema  vipimo vilivyofanyika hivi karibuni hapa nchini hususani katika jiji la Dar es Salaam vinaonyesha kuwa kiwango cha juu cha mawimbi kilichofikiwa kutokana na minara ya mawasiliano iliyopo ni kipimo cha volti 6.02 kwa mita tofauti na kiwango cha juu cha ukomo kisichotakiwa kuzidi ambacho ni Volti 61 kwa mita kilichowekwa na Tume ya Kimataifa ya Kudhibiti Mionzi.

error: Content is protected !!