Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yasisitiza wajawazito kutibiwa bure
Afya

Serikali yasisitiza wajawazito kutibiwa bure

Wajawazito wakiwa hospitalini
Spread the love

SERIKALI imesisitiza kuwa sera ya Afya ya mwaka 2007 inaeleza kuwa huduma za kina mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote zinatakiwa kutolewa bila malipo, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangwala, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Manira Musta Khatib (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua Je, serikali ina mpango gani watafuta tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji kama ilivyofuta za matibabu ya wazee na wagonjwa wa kisukari.

Dk. Kigwangwala amesema serikali haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji.

Amesema huduma hizo zinatolewa katika ngazi zote katika vituo vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za serikali.

“Ili kuhakikisha sera hii inatekelezwa kwa vitendo, wizara inahakikisha akina mama wanakuwa na vifaa muhimu vya kujifungulia, ambapo vifuko maalum vyenye vifaa vya kujifungulia kwa wanawake 500,000 vitasamazwa nchi nzima kulingana na uhitaji.

“Kwa wastani nchi ya Tanzania jumla ya akina mama 1,900,000 wanajifungua kila mwaka,” ameeleza Dk. Kigwangwala.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangwala amesema kuwa kutokana na sera ya afya kwa sasa serikali imejikita zaidi katika kuhimalisha sekta ya afya.

Amesema katika juhudi za kuhakikisha vifo vya akina mama na watoto serikali inajipanga kuhakikisha kila vituo vya afya vyote vya serikali vinatoa vifaa kwa akima mama wajawazito na watoto ili waweze kupatiwa huduma iliyo salama na bora zaidi.

Akiendelea kujibu maswali hayo Dk. Kigwangwala amewataka wabunge pamoja na jamii kuhakikisha wanahakikisha akina mama wajawazito wanapatiwa natibabu bure.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

Afya

573 wafariki kwa kipindupindu

Spread the loveTakriban watu 573 kati ya 11,640 walioambukizwa kipindupindu nchini Nigeria...

error: Content is protected !!