July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yasisitiza uzazi wa mpango

Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya (CCM)

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa elimu ya uzazi wa mipango katika jamii si kazi ya serikali pekee, bali jamii inatakiwa kutambua umuhimu kuzaa kwa mpango ili kuondokana na kuwepo kwa watoto wa mitaani. Anaandika  Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk. Kebwe Steven Kebwe alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya (CCM).

 Bulaya alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa viongozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila ambamo wanapingana na uzazi wa mpango.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Hilda  Ngoye,(CCM)alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuendeleza kampeini za kulinda afya ya wanawake na watoto na kuthibiti ongezeko la watu kiholela.

Akijibu swali hilo Dk.Kebwe amesema  jukumu la kulinda afya ya akina mama na watoto ni jukumu la jamii wenywe.

Dk.Kebwe amesema ni kweli kwa miaka ya nyuma Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,iliendesha kampeini ya nyota ya kijani ambayo ilielimisha jamii juu ya suala zima la mpango wa uzazi kuthibiti ongezeko la watu.

Amesema  kwa sasa serikali pamoja na wadau wa uzazi wa mpango wanaendelea na kampeini ya uhamasishaji wa nyota ya kijani kwa kutumia vyombo vya habari.

error: Content is protected !!