January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yasisitiza pensheni kulipwa

Spread the love

SERIKALI imedhamiria  kusimamia na kuhakikisha michango ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini inalipwa kwa wakati, anaandika Eunice Laurian.

Lengo linalokusudiwa ni kuwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya uendeshaji na ulipaji wa mafao kwa wanachama.

Akifungua mkutano wa 25 wa mwaka kwa wanachama wa mfuko wa pensheni wa PPF na wadau wengine wa wa hifadhi ya jamii leo jijini Dar es Salaam, Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amesema, serikali inatambua umuhimu wa mifuko hiyo na tayari imeanza kulipa madeni ya serikali yanayodaiwa na mifuko.

Amesema serikali imetoa agizo la kuwataka waajiri wote kuhakikisha wana mikataba na wafanyakazi wao kwa kuwaandikisha katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwachangia kama serikali inavyotaka.

“Naagiza kwamba hatua za kisheria zichukuliwe kwa kuwashitaki   wajiri wote wanao chelewesha michango na kuzomba mahakama kuzishughulikia mapema kesi hizo ili kuondoa kero kwa wananchi na mifuko,” amesema Mhe Kijaji.

Pia ameutaka mfuko wa PPF uangalie   uwekezaji katika maeneo muhimu ambayo hayapo katika mfumo uliopo sasa kwa kuzingatia kanuni za uwekezaji zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kujiongezea mapato.

Kwa upande wa Ramadhani Khijjah, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF amaeleza kwamba, kwa sasa dhamani ya mfuko imeongezeka kwa asilimia 40 kutoka shilingi trilioni 1.48 mwaka 2013 hadi kufikia trilioni 2.08 Juni mwaka jana.

“Mfuko wa PPF umekuwa kumapatao na kwa idadi ya wanachama ambapo mpaka mwishoni mwa mwaka 2015 thamani imeongezeka kwa kufikia kiasi cha shillingi trillion 2.23,” amesema Kijaji.

error: Content is protected !!